Shirika la Posta lapiga hatua Kidigitali
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Na Annastazia Maginga, Mwanza
Mfumo w kidigitali na mapinduzi mapya ya biashara ya mtandano umewezesha Shirika la Posta Mkoa wa Mwanza kuongeza idadi ya wateja wake kutoka elfu nane hadi wateja laki tatu.
Hatua  hiyo imekuja baada ya  Shirika hilo kuachana na mfumo wa analogia  na kutumia  mfumo wa kisasa ili kuendana na kasi ya Teknolojia ya  Habari   na Mawasiliano (TEHAMA).
Meneja wa Shirika hilo Mkoa wa Mwanza, Dongwe James Dongwe amesema kwa kutumia mfumo wa kisasa wa Posta Mtandaoni (Smart Posta)  wameweza kuwafikia wateja wengi zaidi ikilinganishwa na wakati wa analogia.
"Mwaka huu  hadi kufikia Septemba, tumewafikia wateja laki tatu ukilinganisha na wateja elfu nane wakati tuliokuwa tukitumia analogia" amesema Dongwe.
Dongwe ameongeza kuwa kupitia simu ya mkononi, mwananchi ataweza kuwa na sanduku la Posta ambapo mfumo huo utamtaarifu mteja kila hatua wakati wa usafirishaji wa mizigo.
"Posta matandaoni (Smart Posta) ni huduma ya simu  zinazopatikana kwa kupakua programu kwenye 'Play Store' na kujisajili kupitia nambari ya simu ambapo gharama kwa mtu binafsi ni Sh.14,200 kwa mwaka  na kampuni au shirika ni 74,000  kwa mwaka" ameeleza Dongwe.
Aidha huduma hiyo inajibu mapungufu yaliyopo ya utumiaji wa sanduku la Posta  ambapo maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) imelifanya shirika hilo kuja  na suluhisho la kila mwenye simu ya mkononi kumiliki sanduku lake  kiganjani.
 
 

 
 
 
 
 
No comments: