LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mfuko wa NHIF waombwa kuweka mpango wa Dunduliza kwa Wanahabari

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Watendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wameombwa kuruhusu mpango wa dunduliza kwa kundi la waandishi wa habari ili kuruhusu waandishi huru wasio na kipato kikubwa waweze kujiunga na mpango wa bima ya afya nchini.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko alitoa ombi hilo mbele ya Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama NHIF, Christopher Mapunda.

Soko alisema zaidi ya asilimia 60 ya waandishi wa habari Tanzania ni waandishi wanaojitegemea hivyo kukiwa na utaratibu wa dunduliza itawasaidia kulipa michango ya bima kwa kiwango kidogokidogo na kukidhi dharama za kupata kadi ya matibabu.

Pia amesema kundi la waandishi wa habari lina changamoto nyingi ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya hivyo kundi hilo likiingizwa kwenye utaratibu huo itawasaidia waandishi wengi.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unatimiza miaka 20 tangu kuanzishwa mwaka 2001 na kwa sasa mfuko unatoa huduma kwa asilimia 8 ya watanzania.

No comments:

Powered by Blogger.