LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mkoani Geita

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenge Maalum wa Uhuru 2021 umewasili katika Mkoa Geita ukitokea mkoani Kagera ambapo mapokezi ya Mwenge huo yamefanyika katika Wilaya ya Bukombe ukitarajiwa kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya tano mkoani humo.

Akipokea Mwenge huo Oktoba 09, 2021, Mkuu wa Mkoa Geita, Rosemary Senyamule amesema utakimbizwa umbali wa kilomita 582.2, kupitia miradi 52 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 18.73 ambapo unatarajiwa kuzimwa na Rais Samia Suluhu Hassan Oktoba 14, 2021 wilayani Chato.

Naye Mkuu wa Wilaya Bukombe, Said Nkumba akipokea Mwenge huo amesema katika Wilaya yake utakimbizwa umbali wa kilomita 86 na kupitia miradi 10 yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.12 kabla ya kukabidhiwa katika Wilaya ya Mbogwe Oktoba 10, 2021.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama picha mbalimbali mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mkoani Geita yaliyofanyika katika Kijiji cha Buganzu wilayani Bukombe ukitokea Biharamulo mkoani Kagera.
Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru 2021 Lt. Josephine Mwambashi akizungumza baada ya kuwasili mkoani Geita.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko akipokea Mwenge wa Uhuru.
Tenki la maji katika mradi wa Buganzu wilayani Bukombe.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Bukombe, Lutengano Mwalwiba akipokea Mwenge wa Uhuru.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.