LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la SAWAU latoa mafunzo kwa wasichana zaidi ya 500 wilayani Ilemela

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Sauti ya Wanawake Ukerewe (SAWAU) limewajengea uwezo zaidi ya wasichana 500 katika Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza kuhusu mbinu mbalimbali za ujasiriamali na afya ya uzazi ambapo matarajio ni wasichana hao kuwa chachu ya mabadiliko kwa wenzao zaidi ya elfu tatu wilayani Ilemela.

Akizunguma kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani mwaka huu 2021, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Sophia Donald amebainisha kuwa hivi sasa wasichana hao wamejitambua na pia wana ujuzi wa kuwasaidia kujikwamua kimaisha hususani dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Wilaya Ilemela, aliyewakilishwa na Afisa Tawala Wilaya Ilemela, Neema Kipeja ambapo aliwaahidi kuwa ofisi yake iko tayari kuwapa ushirikiano wasichana waliopata mafunzo kutoka SAWAU ili kukabiliana na changamoto walizonazo ikiwemo uhaba wa vitendea kazi ikiwemo vyerehani kama walivyoomba kupitia risala yao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Afisa Tawala Wilaya Ilemela akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaua Ilemela, Hassan Masala kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani 2021 yaliyoandaliwa na Shirika la SAWAU.
Mkurugenzi wa Shirika la SAWAU, Sophia Donald (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Shirika la MIBOS (kulia).
Baadhi ya wasichana walipata mafunzo katika Shirika la SAWAU wakionesha baadhi ya bidhaa walizotengeneza.
Wasichana wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wasichana na viongozi mbalimbali.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.