LIVE STREAM ADS

Header Ads

Uzuri wa Tanzania (S01 E17) Mkeka umetulia Buswelu-Sabasaba

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwaka 2018 ujenzi wa barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza yenye urefu wa kilomita 9.7 uligharimu shilingi bilioni 18 ukijumuisha barabara nyingine ambazo ni Isamilo-Big Bite hadi Mji Mwema kilomita 1.2 na Makongoro Junction-Mwaloni mpaka Kigoto Kirumba kilomita 1.2 ukitekelezwa na kampuni ya Sinohydro Corporation LTD.

Pia mwaka 2016 zaidi ya bilioni mbili zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe za Muungano zilibadilishwa matumizi na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Magufuli na kuelekeza zitumike kwenye upanuzi wa barabara ya Makongoro-Airport kutoa njia mbili hadi njia nne kuanzia eneo la Ghana Quarter hadi uwanja wa ndege wa Mwanza.

Fuatilia mwonekano wa kazi iliyofanyika katika barabara hizo kuanzia eneo la Buswelu-Sabasaba ambapo tamati itakuwa mzunguko wa barabara ya Kenyatta/ Rock City.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.