GST yatoa mafunzo kwa wachimbaji wa madini zaidi ya 300 Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mafunzo hayo yalianza rasmi Novemba 27,2021 na kuhitimishwa Disemba 1, 2021 kwa kuwashirikisha wachimbaji kutoka maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa wa Mwanza. Mafunzo kwa vitendo yalifanyika katika Wilaya ya Misungwi na Kwimba katika maeneo ya Mhalo, Mwamazengo , Lishokela na Chatta.
Lengo kubwa la kutoa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na uelewa wa namna bora ya uchukuaji wa sampuli wakilishi kutoka katika maeneo yao ya kazi kwa ajili ya uchunguzi wa maabara pamoja na kuwaelimisha njia na hatua sahihi za utafiti wa Madini katika leseni zao.
Mpaka sasa GST imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania katika mikoa kumi.
Na Samwel Mtuwa - Mwanza
No comments: