LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia aupiga mwingi Sekta ya Elimu, RC Mwanza ashuhudia maajabu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Eng. Robert Gabriel amezindua matumizi ya vyumba vipya vya madarasa ambavyo tayari vimekamilika na kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka huu 2022.

Uzinduzi huo umefanyika Januari 19, 2022 katika Shule ya Sekondari Bujingwa iliyopo Manispaa ya Ilemela ambapo hatua hiyo inatoa fursa kwa wanafunzi 68,789 waliofaulu mtihadi wa darasa la saba kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza.

Eng. Robert ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na miundombinu yake na hivyo kuwahimiza waalimu na wazazi kushirikiana ili kuhakikisha wanaondoa daraja sufuri kwa wanafunzi.

Naye Afisa Elimu Mkoa Mwanza, Mwl. Martin Kwabi amesema Mkoa Mwanza kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 ulipokea shilingi Bilioni 20.5 zilizosaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa 1,017 pamoja na miundombinu yake ambapo vyumba 985 ni vya Sekondari na vyumba 32 ni Shule Shikizi.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Eng. Robert Gabriel (wa pili kushoto) akimpongeza Mkuu wa Wilaya Ilemela Hassan Masala (kulia) kwa kusimamia vyema ujenzi wa vyumba vya madarasa. Katikati ni Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela Modest Apolinary na kushoto ni Afisa Elimu Mkoa Mwanza Mwl. Martin Nkwabe.
Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza Shule ya Sekondari Bujingwa Manispaa ya Ilemela wakiwa darasani.
Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza Shule ya Sekondari Bujingwa wakiwa kwenye moja ya madarasa mapya yaliyojengwa shuleni hapo.
Wanafunzi wa kidato cha Kwanza Shule ya Sekondari Bujingwa wakiwa darasani.
Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wakiwemo waalimu wa Shule ya Sekondari Bujingwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mwanza Eng. Robert Gabriel.
Mwonekano wa vyumba vipya vya madarasa katika Shule ya Sekondari Bujingwa.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.