LIVE STREAM ADS

Header Ads

Balozi Kombo akutana na NGO’s kiitaliano zinazofanya kazi nchini Tanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Na Mwandishi Maalum, Italy
Balozi wa Tanzania nchini Italy, Mahmoud Thabit Kombo amepongeza juhudi za Taasisi binafsi zisizo za Kiserikali (NGO's) za kimaendeleo zinazosaidia jamii kwani zinatoa michango mikubwa ya Kibinadamu kwa Tanzania, ikiwemo kukuza mahusiano ya muda mrefu yaliopo kati ya nchi hizo mbili.

Balozi Kombo amebainisha hayo katika hafla iliyofanyika jioni ya Februari 26,2022 ambapo inakuwa ni mara ya kwanza kukutana na NGO's hizo zaidi ya 65 za Kiitaliano zinazofanya kazi zake nchini Tanzania pamoja na kupokea Ripoti mbalimbali za Miradi iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Balozi Kombo amewahakikishia na kuwahidi kufanya kazi kwa karibu na Mamlaka husika ili kutatua changamoto zilizokuwepo katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayofanyika na inayotarajiwa kufanyika nchini Tanzania.

Awali Balozi Kombo alipokea Kitabu rasmi kilichoandikwa na NGO ya Zawadi kutoka nchini Tanzania ambayo ina Kituo chake cha kulea Mayatima na Watoto wenye Ulemavu.

Ambapo pia NGO hiyo ya Zawadi ilipata wasaha wa kuonesha Filamu na Kitabu cha hatua na mafanikio yaliyofanikiwa katika Mkoa wa Iringa nchini.

No comments:

Powered by Blogger.