LIVE STREAM ADS

Header Ads

Machinga wajivunia kuanzisha SACCOS

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Na Fredy Mgunda, Iringa
Wafanyabiashara wadogo (Machinga) Mkoa wa Iringa wamesema kuwa kuundwa kwa SACCOS ya umoja huo nchi nzima kutawasaidia kupata kwa mitaji na kukuza mitaji yao ya biashara kwa kuwa watakuwa na uhakika wa kukopa kwa riba nafuu.

Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Iringa, Yahaya Mpelembwa amesema wanaenda kuzindua SACCOS ya wafanyabiashara wadogo (Mavchinga) siku ya tarehe 19/02/2022 mkoani Dar es salaam na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa.

Mpelembwa alisema kuwa wanampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suhulu Hassan kwa kuamua kuanzisha SACCOS ya machinga nchi nzima kwa kuwa itasaidia kukuza mitaji ya wafanyabiasha hao.

Alisema kuwa amekuwa Rais wa kwanza kuweka historia ya kukutana kundi hilo la wafanyabiashara wadogo wadogo na kutambua mchango wao katika kukuza uchumi wan chi.

Mpelembwa alisema kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wanakilio cha muda mrefu cha kutokopesheka kwa kuwa walikuwa hawana dhamana hivyo kitendo cha serikali kuanzisha SACCOS hiyo itakuwa mchombozi kwao.

Alisema kuwa kuzinduliwa kwa SACCOS hiyo kutakuwa na faida ya wafanyabishara hao kuanza kukopa kwa riba nafuu tofauti ilivyo hivi sasa ambavyo wanahangaika kupata mitaji ya kukuza biashara zao.

Mpelembwa alisema kuwa wafanyabiashara wadogo wadogo (MACHINGA) mkoa wa Iringa wanaungana na wafanyabiashara hao nchi nzima kukifanya chombo hicho kuwa imara zaidi kwa kuwasaidia mitaji machinga wote.

Alisema kuwa swala la mitaji kwa machinga mkoa wa Iringa kimekuwa kikwazo kikubwa katika kukuza biashara wanazozifanya hivyo kuwepo kwa chombo hicho kutasaidia kukuza mitaji yao.

Nao baadhi ya machinga mkoani Iringa walisema kuwa kuundwa kwa chombo hicho kutasaidia kukuza biashara zao na kuwapelekea kuwa wafanyabiashara wakubwa.

Walisema kuwa wanampongeza na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suhulu Hassan kwa kulikumbuka kundi la machinga ambalo kwa miaka mingi lilikuwa limesaulika na viongozi wengine.

Waliongeza kuwa kuzinduliwa kwa chombo hicho kutasaidia kukuza uchumi wa wafanyabiashara hao na wananchi wote kwa ujumla kwa kusaidia kukuza maendeleo ya nchi na kuongeza pato la wananchi.

No comments:

Powered by Blogger.