LIVE STREAM ADS

Header Ads

MNEC yatoa miezi sita kwa Mwekezani Ilala

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt Samuel Gwamaka amekitaka kiwanda cha Guoyang Biotech Company Ltd kilichopo katika Mtaa wa Kiboga, Kata ya Msongole wilayani Ilala kuhakikisha ndani ya miezi sita wawe wamekamilisha mchakato wa kukamilisha kaguzi ya mazingira (environmental audit) na wawe wamepata cheti.

Ameyasema hayo alipokua katika ziara ya kukagua masuala yote yanayohusu utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika kiwanda hiko ambacho kinalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kwa kusababisha harufu kali ambayo imetishia tishio kwa wakazi wa eneo hilo.
Kiwanda hiko kinahusika na utengenezaji wa dizeli ya viwandani (Industrial diesel) ila kuna tetesi kuwa dizeli hiyo inauzwa kwa wenye vituo vya mafuta kwahiyo NEMC pia katika ziara ilikua ikifuatilia kuhusu tetesi hizo.

“Dizeli hii inayozalishwa hapa haifai kutumika kwenye vituo vya mafuta sababu ina virutubisho vingi visivyofaa ambavyo vikiingia kwenye mafuta husababisha injini kuwa na umri mfupi na kuharibika kwa haraka, nawatahadharisha wenye vituo wasije kununua mafuta haya” Dkt. Gwamaka

Naye Kaimu Meneja kanda ya mashariki kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bwana Emmanuel Lewanga amesema kuwa wako na NEMC katika ziara hiyo ya kutembelea kiwanda tajwa na wao watachukua sampuli ya dizeli inayozalishwa kiwandani hapo, na kwenda maabara kuifanyia uchunguzi kujua kemikali ya aina gani inachanganywa katika mafuta hayo machafu.

No comments:

Powered by Blogger.