LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia apata mapokezi makubwa licha ya mvua kuchachamaa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Mwanza akiwa njiani kuelekea mkoani Mara kwa ajili ya kuhudhuria kilele cha miaka 45 ya CCM. Akiwa jijini Mwanza amesalimiana na wananchi waliojitokeza katika viunga mbalimbali kumlaki.

Akizungumza katika wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Rais Samia ametengua uteuzi wa Wakurugenzi wanne wa Halamashauri za Buchosa- Mwanza, Iringa, Singida na Mbeya kutokana na ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo huku uchunguzi ukiendelea kwa Mkurugenzi wa Geita ambapo amesema naye ikibainika alitumia vibaya fedha za maendeleo naye atatenguliwa.

Aidha Rais Samia amemwagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuunda Tume itakayochunguza tuhuma za jeshi la polisi kuhusika na kifo cha mfanyabiashara wa madini mkoani Mtwara huku akitaka hatua madhubuti kuchukuliwa ili kudhibiti vitendo vya mauaji vinavyoripotiwa nchini.
Tazama matukio mbalimbali katika picha...
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.