LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tanzania Prisons watamba kuwapiga Simba SC kwenye mshono

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania Prisons kikiongozwa na nyota wake Jeremia Juma kimetamba kuwatonesha kwenye 'mshono' mabingwa watetezi Simba SC kwenye mchezo wao wa leo. Tambo hizo zinakuja baada ya Simba kutpoteza michezo miwili mfululizo sawa na Prisons huku ikitoa sare moja.

Pia kikosi hicho kimedai kutokuwa na hofu na ulinzi wa timu ya Simba unaoongozwa na wakongwe Henock Inonga, Pascal Wawa na Joash Onyango kwenye mchezo unaotarajiwa kupigwa Februari 03, 2022 katika dimba la Mkapa.

Juma ni mshambuliaji pekee ambaye amefunga 'hat trick' kwenye ligi msimu wa 2021/22 na aliwatungua Namungo FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.

Prisons iliyo nafasi ya 16 na pointi 11 inakutana na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi 25 zote zikiwa zimecheza mechi 13.

"Hatuogopi kuelekea kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba, tunawatambua na tunajua ni timu imara lakini tunawaheshimu kwa kuwa jambo ambalo tunahitaji ni pointi tatu" amesema Juma na kuongeza;

“Uwepo wa mabeki wao wakongwe haitutishi kwani hata mimi pia kwenye ligi nipo muda mrefu na nina uzoefu wa kutosha kikubwa ni kusubiri na kuona baada ya dakika 90 hali itakavyokuwa” amesisitiza Juma.

Msimu wa 2021/22 walipokutana uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-1 Prisons na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

No comments:

Powered by Blogger.