LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wizara ya Afya yatoa mafunzo kwa wanahabari kuhusu Chanjo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kwenye kikao cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga kuhusu uhamasishaji wa masuala ya chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya UVIKO - 19.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waandishi wa habari wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha masuala ya chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo dhidi ya UVIKO -19.

Rai hiyo imetolewa Ijumaa Februari 4,2022 na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile wakati wa mafunzo ya waandishi wa habari wa mikoa ya Shinyanga na Simiyu kwa ajili ya uhamasishaji kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo chanjo ya Chanjo ya UVIKO – 19 ili kulinda afya za wananchi.

Dkt. Ndungile alisema kuwa waandishi wanayo nafasi kubwa ya kutoa habari na kuwahamasisha wananchii kuhusiana na chanjo kwani wananchi wana imani na vyombo vya habari.

"Msiishie kuandika stori ya leo tu bali mkawe mabalozi wa kuandika habari za chanjo kila mara. Naomba mkawe mstari wa mbele kuhamasisha masuala ya chanjo na wale ambao hawajachanja wachanje ili wawe chachu ya mabadiliko kwani wana wajibu wa kufikisha taarifa sahihi kwa jamii" alisema Dkt. Ndungile.

“Tumekutana hapa kujadili kuhusu chanjo na wajibu wa mwandishi wa habari kuhamasisha masuala ya chanjo. Kikao cha leo kikazae matukio mbalimbali ya chanjo. Tumeona kuna chanjo zaidi ya 10 hivyo unaweza ukawa unazungumzia chanjo moja kila mwezi mfano chanjo ya kuzuia chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi” alisema Dkt. Ndungile.

Alizitaja miongoni mwa chanjo zinazotolewa nchini Tanzania ni pamoja na chanjo ya UVIKO - 19, Kifua Kikuu (BCG),Polio (OPV), Polio (IPV), Surua Rubela (MR), (Donda koo,kifaduro,pepo punda, homa ya ini homa ya uti wa mgongo, homa ya mapafu -Pentavalent), Pepo punda kwa wajawazito, saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV), Nimonia (PCV13) na Kuhara Kukali ( Rota).

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo waliiomba Serikali kushirikiana kwa ukaribu na waandishi wa habari kwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara bila kuyasahau makundi mengine katika jamii wakiwemo viongozi wa dini, siasa,mila na wasanii wa nyimbo za asili kwani wana ushawishi mkubwa katika jamii.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kwenye semina hiyo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kwenye semina ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga kuhusu uhamasishaji wa masuala ya chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya UVIKO - 19
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Afya, Catherine Sungura akizungumza kwenye semina hiyo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye semina ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga kuhusu Uhamasishaji wa masuala ya chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya UVIKO - 19
Afisa Mpango wa Taifa wa Chanjo - Wizara ya Afya, Lotalis Gadau akitoa mada kuhusu chanjo mbalimbali kwenye mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga kuhusu masuala ya chanjo.

Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Waandishi wa habari wakiwa kwenye semina ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga kuhusu Uhamasishaji wa masuala ya chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya UVIKO - 19.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye semina ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga kuhusu Uhamasishaji wa masuala ya chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya UVIKO - 19
Mratibu wa Chanjo ya UVIKO- 19 Mkoa wa Shinyanga, Timothy Sosoma akiwa ukumbini
Waandishi wa habari wakiwa kwenye semina ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu na Shinyanga kuhusu Uhamasishaji wa masuala ya chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya UVIKO - 19.

No comments:

Powered by Blogger.