LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ya CRDB yatambulisha huduma ya Al-Barakah jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Benki ya CRDB imetambulisha huduma ya ‘Al-Barakah Banking’ kwa waumini wa dini ya kiislamu jijini Mwanza na kuwahimiza kujiunga na huduma hiyo ili kunufaika na huduma za kifedha ikiwemo mikopo bila riba inayoendana na imani yao.

Huduma hiyo imetambulishwa Machi 24, 200 kwenye kongamano liowashirikisha viongozi wa BAKWATA kuanzia ngazi ya misikiti, Kata, Wilaya na Mkoa Mwanza ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye mbio za riadha zilizoandaliwa na Jumuiya ya Vijana wa BAKWATA zitakazofanyika jumapili Machi 27, 2022 jijini Mwanza zikidhaminiwa na benki ya CRDB.

Akizungumza kwenye kongamano hilo, Meneja Biashara wa CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanally aliwahimiza waumini wa dini ya kiislamu kuchangamkia fursa zinazotolewa na benki hiyo kupitia huduma ya Al-Barakah kwani kwa muda mrefu wamekosa huduma za kibenki ikiwemo mikopo kutokana na riba kwao kuwa haramu kulingana na misingi ya Sharia za dini hiyo.

Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke alisema ujio wa huduma ya ‘Al-Barakah Baking’ ni suluhisho kwa waislamu kutunza fedha zao kwenye mitungi na hivyo kuagiza waumini wa dini ya kiislamu na misikiti mkoani Mwanza kufungua akaunti za Al-Barakah ili kunufaika na huduma za kifedha ikiwemo kujiwekea akiba pamoja na mikopo bila riba.

Akifungua kongamano hilo, Mkuu wa Wilaya Ilemela Hassan Masala aliwaasa wananchi kujenga utamaduni wa kitunza akiba kupitia taasisi za kifedha ikiwemo benki ya CRDB kwa manufaa ya sasa na baadae huku wakichangamkia fursa ya mikopo bila riba kupitia huduma ya Al-Barakah ili kukuza shughuli zao za kiuchumi.

Masala pia aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuhamasisha waumini wao kupata chanzo ya UVIKO-19 kwani ugonjwa huo bado upon a unahatarisha maisha ya wale ambao hawajachanja ambapo aliungana na Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke kusisitiza kuwa chanjo zote zilizoletwa nchini ni salama na hazina madhara. Aliwahimiza pia kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi kujiandaa na zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu 2022.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Ilemela mkoani mwanza, Hassan Masala akifungua kongamano baina ya benki ya CRDB na BAKWAMA mkoani Mwanza ambapo pamoja na mambo mengine benki ya CRDB ilitumia kongamano hilo kutambulisha huduma yake ya 'Al-Barakah Banking' ambayo mteja anaweza kukopa bila riba.
Mkuu wa Wilaya Ilemela, Hassan Masala akizungumza kwenye kongamano hilo.
Meneja Biashara benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly alisema huduma ya Al-Barakah inatoa fursa kwa waumini wa dini ya kiislamu kupata huduma za kifedha ikiwemo mikopo bila riba ili kuendana na imani yao.
Washiriki wakifuatilia kongamano hilo.
Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke aliwahimiza waumini wa dini ya kiislamu na wasio waumini wa dini hiyo kuchangamkia fursa zinazotolewa na benki ya CRDB kupitia huduma ya Al-Barakh ikiwemo mikopo bila riba.
Washiriki wakifuatilia kongamano hilo.
Washiriki ambao ni viongozi mbalimbali wa BAKWATA kuanzia ngazi ya ngazi mkoani Mwanza wakiwa wakifuatilia kongamano hilo.
Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.
Meneja Mwandamizi wa Sheria kutoka benki ya CRDB, Muhsin Said akiwasilisha mada kuhusu huduma ya 'Al-Baraka Banking' kwenye kongamano hilo.
Washiriki wakifuatilia mada kwenye kongamano hilo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.