LIVE STREAM ADS

Header Ads

CRDB yawakutanisha wateja wake Mwanza, wahimizwa kuchangamkia mikopo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Benki ya CRDB imewahimiza wateja wake jijini Mwanza kuongeza wigo wa kuchangamkia fursa za mikopo zinazotolewa na benki hiyo ambapo mteja mmoja anaweza kukopa hadi shilingi bilioni 233 huduma ambayo haipatikani katika mabeki mengine.

Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Benki ya CRDB, Mussa Lwila aliyasema hayo Machi 16, 2022 wakati akizungumza na wateja wa benki hiyo kwenye hafla ya chakula cha jioni iliyowajumuisha wafanyakazi wa benki na wateja jijini Mwanza.

"Kwa mtaji wetu tunaruhusiwa kumkopesha mteja mmoja hadi shilingi bilioni 233, kwa nini usiwe wewe?" alihoji Lwila akiwahamasisha wateja wa benki ya CRDB kuchangamkia huduma ya mikopo katika benki hiyo ili kukuza mitaji yao.

Mkurugenzi wa Uendeshaji Matawi Benki ya CRDB, Boma Raballa aliwahakikishia huduma bora wateja wa benki hiyo ambapo katika huduma ya mikopo alisema mteja mpya akiwasilisha maombi yake atapata majibu ndani ya siku 14 huku mteja mpya akipata majibu ndani ya siku saba na hivyo kuwapunguzia upotevu wa muda.

Naye Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly alisema kwa wateja ambao wana tenda za kusambaza bidhaa katika makampuni mbalimbali ikiwemo ya ujenzi ama migodi wanaweza kupata dhamana kupitia benki hiyo na kupata bidhaa zenye thamani hadi shilingi bilioni mbili bila mteja kuweka dhamana ya mali yake kama vile nyumba ama kiwanja.

Kwa upande wake Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta aliwahimiza wateja wa benki hiyo hususani waajiri kutumia huduma ya 'Simu Banking' ili kurahisisha shughuli zao ikiwemo kufanya malipo yao akisema huduma hiyo imeboreshwa zaidi na ina usalama mkubwa.
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa akizungumza kwenye hafla hiyo.
Meneja Biashara CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly.
Wateja wa CRDB pia wameshauriwa kujiunga na huduma ya bima inayotolewa na benki hiyo ikiwemo bima ya afya, magari na majanga ambapo akipata majanga anapata huduma ndani ya siku tano.
Meneja wa CRDB Tawi la Mwanza, Jeremiah Msemo akiwakaribisha wateja kwenye hafla hiyo.
Wateja wa CRDB jijini Mwanza wakifuatilia hafla hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha cha Mikopo Benki ya CRDB, Mussa Lwila akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wateja wa CRDB wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uendeshaji Matawi Benki ya CRDB, Boma Raballa.
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta (kushoto) akiwatambulisha mameneja wa matawi ya benki hiyo jijini Mwanza.
Wateja wa CRDB jijini Mwanza wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wateja wa CRDB jijini Mwanza.
Wateja wa CRDB wakiwa kwenye mchaparo jijini Mwanza.
Wateja wa CRDB.
Viongozi wa CRDB wakibadilishana mawazo na wateja.

No comments:

Powered by Blogger.