LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwanza wamshukuru Rais Samia utekelezaji wa miradi ya maji

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel (katikati) akifungua koki ya maji kama ishara ya kuanza kutumia rasmi kwa mradi wa maji Sayaka uliopo katika Kijiji cha Sayaka wilayani Magu ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani. 

Mradi huo umekamilika kwa asilimia 97 ukitekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa gharama ya shilingi milioni 270 ambapo tayari zimetumika shilingi milioni 232.5.

Mhandisi Robert Gabriel ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi ya maji ambapo katika Mkoa Mwanza RUWASA imetengewa shilingi bilioni 18 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 23 ya maji akisema "Rais Samia anaupiga mwingi".
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Magu (kushoto) akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha Sayaka kama ishara ya kukamilika kwa mradi wa maji Sayaka na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Ribert Gabriel akipanda ngazi kukagua tenki la maji katika mradi wa maji Sayaka wilayani Magu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akipanda mti kwenye chanzo cha mradi wa maji Sayaka wilayani Magu ikiwa ni jitihada za kuhamasisha wananchi kutunza vyanzo vyanzo vya maji.
Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kalli akipanda mti katika chanzi cha mradi wa maji Sayaka.
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Magu akipanda mche kwenye chanzo cha mradi wa maji Sayaka.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza kwenye uzinduzi wa Wiki ya Maji uliofanyika katika Kijiji cha Sayaka wilayani Magu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara kwenye uzinduzi wa Wiki ya Maji uliofanyika katika Kijiji cha Sayaka wilayani Magu.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli akitoa salamu kwa wananchi kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Maji yaliyofanyika katika Kijiji cha Sayaka wilayani humo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Magu akitoa salamu za chama kwenye uzinduzi huo.
Diwani wa Kata ya Lubugu wilayani Magu akitoa shukurani kwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukamilisha mradi wa maji Sayaka na kuwaondolea adha wananchi kutembea umbali mrefu kwenda kusaka maji visimani.
Wananchi katika Kijiji cha Sayaka wilayani Magu wakifuatilia uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani ambapo kwa Mkoa Mwanza uzinduzi huo umefanyika Machi 18, 2022. Itakumbukwa Wiki ya Maji Duniani huadhimishwa kuanzia Machi 16 hadi 22 kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.