LIVE STREAM ADS

Header Ads

Arusha wazidi kuboresha mioundombinu ya elimu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella.


Na Rose Jackson, Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema Mkoa huo umetenga fedha kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri jumla ya shilingi Milioni 884.15 kwa kipndi cha mwezi Julai hadi Februari 2022 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu 158 katika Shule za Msingi.

Mongela aliyasema hayo katika kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kuanzia mwezi Julai 2021 hadi mwezi Februari 2022.

Alisema pia Mkoa umetenga shilingi bilioni 1.92 fedha za UVIKO - 19 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 96 ya shule shikizi ili kuondoa adha ya mtoto wanaosoma kutembea umbali mrefu kwa kila halmashauri.

Alieleza kuwa Mkoa umetenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi ili kuhakikisha wanafunzi qananufaika na elimu bila malipo.

Aidha alisema katika kipindi cha miezi 6 cha utekelezaji wa Ilani jumla ya shule mpya 14 zimeongezeka kutoka shule 823 mwaka 2021 hadi kufikia shule 837 mwezi Februari 2022 ikiwa ni shule za msingi huku upande wa shule za sekondari kukiongezeka kwa shule mpya 17 kutoka shule 252 hadi kufikia shule 269 Februari 2022.

Awali Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Dkt. Athuman Kihamia aliwakumbusha watendaji walioteuliwa na Serikali kuwa waadilifu, wawajibikaji na ambao watazifanya rasilimali kuonyesha matokeo chanya huku wakiyafanya madaraka ya umma kuwa msingi wa maamuzi sambamba na kuwa wafuatiliaji na watathimini katika utekelezaji wa mipango wanayoipanga.

No comments:

Powered by Blogger.