LIVE STREAM ADS

Header Ads

Majeruhi wa ajali iliyohusisha wanahabari wa Mwanza wanaendelea vyema

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Eng. Robert Gabriel (kulia) amemtembelea mwanahabari wa Icon Online TV, Vanny Charles (kushoto) ili kumjulia hali. Mwanahabari huyo ni miongoni mwa majeruhi waliopata ajali iliyotokea Januari 11, 2022 katika Wilaya ya Busega wakielekea Ukerewe kupitia Bunda.

RC Gabriel alifurahishwa na maendeleo mazuri kiafya ya mwanahabari huyo na kutumia fursa hiyo pia kuwaombea majeruhi wote akiwemo mwanahabari mwingine Tunu Herman ili wapone na kurejea kwenye majukumu ya kulijenga Taifa.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Eng. Robert Gabriel (wa tatu) pamoja na ujumbe alioambatana nao akiwa kwenye picha ya pamoja na mwanahabari wa Icon Online TV, Vanny Charles (wa pili kushoto) baada ya kumtembelea nyumbani kwake.
SOMA>>> 

No comments:

Powered by Blogger.