LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mtandao wa TGNP washiriki Kongamano la Siku ya Wanawake jijini Arusha

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeshiriki Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jumatatu Machi 07, 2022 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha kwa lengo la kuwakutanisha Wanawake na wadau wengine katika kujadili changamoto zinazowakabili Wanawake na Ustawi wao.

Kongamano hilo limeongozwa na kauli mbiu ‘Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu, Tujitokeze kuhesabiwa’.

Akifungua Kongamano hilo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mapinduzi makubwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake kwa kuwezesha wanawake kufikia kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu.

Mpanju amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia kumefanyika mapinduzi makubwa na hatua kubwa imepigwa katika kujenga kizazi cha haki na usawa huku wanawake wakichaguliwa na kuteuliwa kuongoza Idara nyeti katika taifa.

“Wanawake ni nguzo ya maendeleo duniani. Ndani ya mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Samia tumepiga hatua kubwa ndani ya mwaka mmoja, tuna Rais Mwanamke, Spika wa Bunge Mwanamke, Katibu Mkuu wa Bunge mwanamke, tuna Mawaziri wanawake 9 katika Wizara nyeti wanafanya kazi vizuri na maendeleo tunayaona, mambo yanakwenda vizuri” amesema Mpanju.

Mpanju amewataka wadau na wananchi kwa ujumla kuwa tayari kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii ikiwemo ukeketaji kwa watoto wa kike akiongeza kuwa ni vyema jamii ikapambana na vitendo vya ukatili hasa dhidi ya Wanawake ili kutorudisha nyuma juhudi za Serikali na wadau za kuleta Usawa wa kijinsia.

Amesema jamii inatakiwa kusimama katika kupambana na kupinga Mila hasi za kumnyima mwanamke haki na kumkandamiza katika kupata fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye jamii ili kumuwezesha mwanamke kuwa na uwezo wa kutatua changamoto zinazomkabili.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jumatatu Machi 7,2022 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi (kulia) akifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Wanachama wa TGNP, Gemma Akilimali (kushoto) na Jovitha Mlay wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Wanachama wa TGNP, Gemma Akilimali (kushoto) na Jovitha Mlay wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi (wa pili kushoto) akiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Mwanachama wa TGNP, Gemma Akilimali akiandika dondoo muhimu kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika  Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Wadau wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika Jijini Arusha.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

No comments:

Powered by Blogger.