LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanawake 'PGA Mwanza City Centre' watoa msaada Shule ya Msingi Sahara

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wanawake kutoka Kanisa la Philadephia Gospel Assembly (PGA) Mwanza City Centre wamekabidhi zawadi za mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Sahara iliyopo jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2022.

Makamu Mkurugenzi wa Idara ya Wanawake na Watoto wa Calvary kutoka Kanisa hilo, Mchungaji Rose Brown amesema zawadi hizo ambazo ni daftari, kalamu na taulo za kike zitawasaidia wanafunzi hususani wa kike ili kujistiri wakati wa hedhi.

Makamu Mwenyekiti wa Idara hiyo ya Calvaly, Sarah Thomas amesema zawadi hizo mbali na kwamba zimetolewa kama sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lakini pia ni kuunga mkono jitihada za Serikali za kutoa elimu bora kwa kila mwanafunzi kwa kujenga madarasa na kuajiri waalimu.

Naye Dkt. Joyce Mihayo kutoka Idara ya Calvary ya Kanisa la PGA Mwanza City Centre ambaye pia ni Mtaalam wa Afya amesema msaada wa zawadi hizo pia unatoa fursa ya kuutangaza Upendo wa Yesu Kristo ambao umewaongoza wanawake wa Idara hiyo na kuwiwa kuwasaidia wanafunzi wa Shule hiyo ambayo iko jirani na Kanisa hilo.

"Mbali na hilo pia tumekuja kutoa elimu ya kijinsia kwa watoto wa darasa la sita na la saba kwa sababu wako katika hatua ya ukuaji ambapo wanakutana na changamoto mbalimbali ikiwemo za kihisia na mihemuko ili tuwasaidie kujitambua na kujisimamia katika kupambana na changamoto hizo na watimize malengo yao" ameeleza Dkt. Mihayo.

Akipokea msaada huo, Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Sahara Mwl. Beatha Lema amesema msaada wa zawadi hizo ikiwemo taulo za kike utaleta chachu kwa wanafunzi wa kike wanaoingia kwenye hatua ya makuzi ambao wanatoka katika familia ambazo wazazi hawaoni umuhimu wa matumizi ya taulo hizo na hivyo kuleta hamasa ya kuwanunulia taulo hizo hatua itakayowasaidia kutokosa masoko wakati wa hedhi.

"Mmetusaidia pedi (taulo za kike) zitatusaidia hususani wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu na hivyo kuwa wasafi (nadhifu) wakiwa shuleni" amesema Elizabeth Bundala ambaye ni mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Sahara wakati akitoa shukurani kwa niaba ya wenzake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Mission jijini Mwanza, Mussa Fereji amewapongeza wanawake wa Kanisa la PGA Mwanza City Centre kwa kutoa zawadi hizo na kutoa rai wadau wengine hususani wanaofanya shughuli za uzalishaji katika Mtaa wake kuiga mfano huo na kuwa na utamaduni wa kuwajibika kwa jamii hususani kuwasaidia wanafunzi kutimiza ndoto zao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Sahara Mwl. Beatha Lema (kulia) akipokea zawadi kwa ajili ya wanafunzi wa Shule hiyo kutoka kwa wanawake wa Kanisa la PGA Mwanza City Centre.
Wanawake wa Kanisa la PGA Mwanza City Centre wakitoa zawadi za mahitaji mbalimbali katika Shule ya Msingi Sahara jijini Mwanza.
Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Sahara Mwl. Beatha Lema (kushoto) akipokea zawadi kwa ajili ya wanafunzi wa Shule hiyo kutoka kwa wanawake wa Kanisa la PGA Mwanza City Centre.
Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Sahara Mwl. Beatha Lema (kulia) akikabidhi zawadi zilizotolewa na wanawake wa Kanisa la PGA Mwanza City Centre kwa wanafunzi wa Shule hiyo.
Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Sahara Mwl. Beatha Lema (kushoto) akikabidhi zawadi zilizotolewa na wanawake wa Kanisa la PGA Mwanza City Centre kwa wanafunzi wa Shule hiyo.
Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Sahara Mwl. Beatha Lema (kulia) akikabidhi zawadi zilizotolewa na wanawake wa Kanisa la PGA Mwanza City Centre kwa wanafunzi wa Shule hiyo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.