LIVE STREAM ADS

Header Ads

Siku 365 za Rais Samia, aweka rekodi mpya Nyamagana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Vyumba 103 vya madarasa yakiwemo maghorofa vimejengwa katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani ikiwa ni rekodi ambayo haijawahi kufikiwa hapo awali.

Hayo yameelezwa Machi 16, 2022 na Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi cha siku 365 (mwaka mmoja) za Rais Samia Suluhu Hassan.

Makilagi amesema Rais Samia Suluhu Hassan amevunja rekodi kwa kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu na hivyo kuondoa adha kwa wanafunzi kubanana madarasani pamoja na michango waliyokuwa wakiitoa wazazi ili kujenga vyumba vya madarasa.

Aidha Makilagi ameongeza kuwa katika siku 365 za Rais Samia, shilingi bilioni 1.3 zimetolewa kama mikopo kwa ajili ya vikundi vya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu katika Wilaya ya Nyamagana na kusaidia wanufaika zaidi ya 1,800 kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za uzalishaji mali.

Katika hatua nyingine Makilagi amepongeza Rais Samia kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miradi ya kimkakati wilayani Nyamagana ikiwemo ujenzi wa stendi ya kisasa Nyegezi pamoja na meli mpya ya MV. Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.