LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau wa Pamba Afrika kukutana jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wadau mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika yanayounda Jumuiya ya Pamba (ACA) wanatarajiwa kukutana jijini Mwanza kwenye mkutano unaolenga kujadili maendeleo ya zao hilo na kuweka mikakati ya pamoja ya kupanua wigo wa soko lake duniani.

Akizungumza na wanahabari jijini Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) ambaye pia ni Rais wa Jumuiya ya Pamba Afrika, Marco Mtunga amesema mkutano huo wa siku mbili kuanzia Machi 17, 2022 pia utahudhuriwa na makampuni makubwa ya ununuzi pamba duniani.

Naye Katibu Mkuu wa ACA kutoka nchini Mali, Fahaca Adeyemi amesema nchi za Afrika Magharibi zimepiga hatua kwenye ulazishaji wa zao la pamba hivyo pamoja na mambo mengine mkutano huo utasaidia mataifa mengine ikiwemo Tanzania kubadilishana mbinu za kukuza uzalishaji wa zao hilo na kuwaimarisha kiuchumi wakulima.

Kwa upande wake Balozi wa Pamba Tanzania, Aggrey Mwanri amesema jitihada mbalimbali ikiwemo utoaji elimu kwa wakulima namna ya kuandaa mashamba na kupanda mbegu kwa kuzingatia vipimo hatua itakayosaidia kuvuna mazao kwa tija hadi kufikia kilo 2,500 kwa hekari moja hatua ambayo tayari imefikiwa na mataifa ya Mali, Misri na Burkna Faso.
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serikali kutoka mikoa inayozalisha zao la pamba nchini Tanzania pia wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo ambao pia Rais wa ACA, Marco Mtunga atautumia kukabidhi urais wa pamba barani Afrika kwa Taifa la Chad.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.