Bodi ya Pamba yawaonya wanaohujumu usambazaji wa viuadudu
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kaimu Mkurugenzi wa TCB, James Shimbe (pichani juu) ametoa onyo hilo Februari 25, 2022 jijini Mwanza wakati wa zoezi la kupokea viuadudu vitakavyosambazwa kwa wakulima wa zao la pamba huku akiwataka Viongozi wa AMCOS ya Chato mkoani Geita waliokimbia uchunguzi kujisalimisha.
Mwakilishi wa kampuni ya Bens Agrostar, Benson Mwalunenge amewahimiza wakulima kufuata ushauri wa kitaalamu kabla ya kutumia viuadudu kwani baadhi yao wamekuwa wakikiuka masharti na hivyo kushindwa kufanya kazi vyema. Kampuni ya Bens Agrostar ilishinda zabuni ya kuagiza viuadudu kwa niaba ya TCB.
Mzigo wa viuadudu kwa ajili ya zao la pamba ukishushwa katika yadi ya TCB Igogo jijini Mwanza.
Mzigo wa viuadudu kwa ajili ya zao la pamba ukishushwa katika yadi ya TCB Igogo jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> Habari zaidi hapa
No comments: