LIVE STREAM ADS

Header Ads

PICHA: Mapokezi ya Jaji Joseph Sinde Warioba jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania (mwaka 1985 hadi 1990), Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (kulia) baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza, Machi 16, 2022 akiwa njiani kuelekea Chato mkoani Geita kuhudhuria maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa Rais ya Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli yatakayofanyika Machi 17, 2022. 
Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba (katikati) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (kulia) baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akiwa njiani kuelekea Chato mkoani Geita.
Viongozi mbalimbali wanaelekea Chato mkoani Geita kupitia uwanja wa ndege wa Mwanza kuhudhuria kumbukizi yakifo cha Hayati Dkt. John Magufuli aliyefariki Machi 17, 2021kutokana na maradhi ya moyo.
'Karibu Mwanza' salamu kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, Ramadhan Ng'anzi (kulia).
'Mwanza ni salama na Kazi Inaendelea'- Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel.
'Mama karibu sana Mwanza'
Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayuko pichani) anatarajiwa kuwaongoza watanzania na wageni mbalimbali kwenye kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha Hayati John Magufuli, Machi 17, 2022 Chato mkoani Geita.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma (katikati) pia amewasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza kuungana na viongozi mbalimbali kuelekea Chato mkoani Geita kuhudhuria kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha Hayati Dkt. John Magufuli, Machi 17, 2022.

No comments:

Powered by Blogger.