LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watu wenye furaha Tanzania wako Mwanza, changamkieni fursa- RC Gabriel

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel amewata wadau mbalimbali kuchangamkia fursa zinazopatikana jijini Mwanza hususani kuchangamkia viwanja katika eneo la ujenzi wa mji mpya na wa kisasa Afrika Mashariki na Kati.

Mhandisi Gabriel ameyasema hayo wakati akifunga kongamano la Siku ya Haki za Mtumiaji Duniani lililofanyika kitaifa jijini Mwanza Machi 15, 2022 likiandaliwa na Tume ya Ushindaji Tanzania (FCC).

Aidha Mhandisi Gabriel ameongeza kuwa Mwanza ni Mji unaokua zaidi kiuchumi barani Afrika na inaendesha shughuli zake kidijitali bila vikwazo na hivyo kuwakaribisha wawekezaji akisema Mwanza ni Jiji ambalo watu wake wana furaha zaidi nchini Tanzania.
Wadau mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel wakati akihitimisha kongamano la Siku ya Mtumiaji Duniani 2022.
Washiriki wakifuatilia kilele cha Siku ya Mtumiaji Duniani 2022.
Wadau wakifuatilia kongamano hilo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.