LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mwanza akutana na Balozi wa Namibia, amhakikishia fursa za uwekezaji

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (kulia) akimkabidhi zawadi ya picha ya jiwe la Bismark (Bismarck Rock) Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Mhe. Lebbius Tobias (kushoto). Jiwe la Bismarck lililopo eneo la Kamanga katika fukwe za Ziwa Victoria jijini Mwanza ni miongoni mwa vivutio vya utalii kwa wazawa na wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel (kulia) akiteta na Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Mhe. Lebbius Tobias (kushoto). 
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Mhe. Lebbius Tobias (kushoto) akiteta na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (kulia) alipofika ofisini kwake.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Namibia nchini Tanzania Mhe. Lebbius Tobias (kulia) ofisini kwake.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amefanya mazungumzo na Balozi wa Namibia nchini Tanzania Mhe. Lebbius Tobias na kumhakikishia uwepo wa fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana jijini Mwanza ambazo zinazoweza kuimarisha ushirikiano zaidi baina ya mataifa yote mawili.

Mhandisi Gabriel amekutana na Balozi Tobias jijini Mwanza Machi 15, 2022 na kumweleza kuwa jiji la Mwanza lina fursa mbalimbali za uwekezaji ikiwemo katika sektaya uvuvi kupitia uwepo wa Ziwa Victoria pamoja na utalii kupitia vivutio vilivyopo jijini Mwanza pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo inafikika kwa urahisi zaidia kwa njia ya anga na barabara kutokea jijini Mwanza.

Naye Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Mhe. Lebbius Tomas amesema kumekuwa na ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na Namibia tangu enzi za kupigani Uhuru katika nyanja za kisiasa hivyo ni wakati mwafaka pia kwa mataifa hayo kukuza ushirikiano zaidi katika nyanja za kiuchumi tofauti na ilivyo sasa hususani ambapo ameahidi nchi kushirikiana na Jiji la Mwanza katika sekta ya uvuvi.

No comments:

Powered by Blogger.