LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wizara ya Maendeleo ya Jamii yatoa mafunzo kwa Viongozi wa Machinga Tanzania (SHIUMA)

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imeandaa mafunzo kwa Viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) kuanzia ngazi ya Wilaya, Mikoa na Taifa kwa lengo la kuwajengea uwezo kutimiza vyema wajibu wao wa kujiletea maendeleo.

Mafunzo hayo ya siku nne kuanzia Mei 16, 2022 yanafanyika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo ni Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Dorothy Gwajima.

Awali akitoa nasaha kwa viongozi wa SHIUMA, Katibu Mkuu wa Wizaa ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk. Zainab Chaula amewataka machinga nchini kuwa wamoja, wazalendo na kutokubali kutumia kwa maslahi ya baadhi ya watu wasiowatakia mema.

Dkt. Chaula amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa wafanyabiashara wadogo katika kukuza uchumi wa taifa ndiyo maana inaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara zao.

Naye Katibu Mkuu SHIUMA, Venatus Anatory amesema mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana kwa karibu na SHIUMA ili kuwasaidia viongozi wa shirikisho hilo kupata uelewa wa pamoja na kwenda kuwaelimisha machinga wenzao ili kuboresha utekelezaji wa shughuli zao.

Mafunzo hayo yamewashirikisha viongozi zaidi ya 500 kutoka Tanzania Bara na Visiwani yakiwa na kaulimbiu isemayo "Machinga ni Fursa Sahihi ya Kukuza Uchumi wa Nchi Yetu".
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katibu Mkuu wa Wizaa ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk. Zainab Chaula akizunumza na viongozi wa SHIUMA jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa SHIUMA Tanzania, Matondo Masanja akisalimia washiriki wa mafunzo hayo.
Katibu Mkuu SHIUMA Tanzania, Venatus Anatory akisalimia washiriki wa mafunzo hayo.
Naibu Katibu Mkuu SHIUMA Tanzania, Joseph Mwanakijiji akisalimiana na washiriki wa mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa SHIUMA Tanzania, Matondo Masanja (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizaa ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk. Zainab Chaula (kulia).
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.