LIVE STREAM ADS

Header Ads

Machinga wamshukuru Rais Samia baada ya kuahidiwa Milioni 10 kila Mkoa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA), Matondo Masanja amemshukuru kwa dhati kubwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuahidi kutoa shilingi milioni 10 kila mkoa nchini ili kusaidia uendeshaji wa shughuli za shirikisho hilo.

Masanja ametoa shukurani hizo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa shirikisho hilo kuanzia ngazi ya wilaya, mikoa na taifa yanayofanyika jijini Dodoma. Masanja pia ameishukuru Serikali kwa kutoa jengo kwa ajili ya ofisi za makao makuu ya SHIUMA Taifa.

Katika mafunzo hayo, Rais Samia alimpigia Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dkt. Gwajima na kuzungumza LIVE na washiriki wa mafunzo hayo na kuahidi kutoa kiasi hicho cha shilingi milioni 10.

Akifungua mafunzo hayo, Waziri Dkt. Gwajima amesema Serikali inakamilisha mfumo wa kuwatambua machinga nchini na kuwakabidhi vitambulisho vilivyoboreshwa vitakavyowasaidia kufanya shughuli zao vyema bila kukimbizana na vyombo vya dola ambapo amewasili kuzingatia taratibu zilizowekwa.

Awali Kaimu Katibu Mkuu SHIUMA, Joseph Mwanakijiji aliomba Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya maeneo rasmi waliyohamishiwa pamoja na kuwarasimishia maeneo hayo ili kupata fursa hatua itakayosaidia kuaminika na kukopesheka katika taasisi za kifedha ili kukuza mitaji yao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa SHIUMA Tanzania, Matondo Masanja akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akifungua mafunzo ya siku nne kuanzia Mei 16-19, 2022 kwa viongozi wa SHIUMA yanayofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akifungua mafunzo hayo.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maluum Mwanaidi Khamis akitoa salamu zake wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ambapo aliwahimiza machinga nchini kushikamana na kumuunga mkoro Rais Samia kutokana na jitihada zake za kuboresha mazingira ya wao kufanyia shughuli zao.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Neema Lugangila akitoa salamu wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Viongozi mbalimbali machinga wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo hayo.
Machinga wakimpongeza Rais Samia kwa 'style' ya mchezaji wa Yanga, Mayele wakimaanisha ameupiga mwingi baada ya kuwaahidi shilingi milioni 10 kila Mkoa ili kuboresha ofisi zao.
Shangwe likiendelea katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.