LIVE STREAM ADS

Header Ads

Madiwani Mwanza waitaka Serikali kutatua changamoto za wananchi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Baadhi ya madiwani Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
***

Na Hellen Mtereko, Mwanza
Madiwani katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza wameitaka Serikali kuongeza nguvu na kuzitatua kwa wakati changamoto za elimu, afya na miundombinu wanazoziwasilisha kwenye baraza la Halmashauri hiyo kwa niaba ya wananchi.

Wametoa kauli hiyo Ijumaa Juni 03, 2022 wakazi wa kikao cha Baraza la Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo pamoja na mambo mengine kimelenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika ngazi ya Kata.

Miongoni mwa madiwani waliowasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi na na changamoto ni diwani wa Kata ya Kishiri, Haruna Maziku aliyesema Mtaa wa Kanenwa una watoto wengi wanaotembea umbali mrefu kwenda shule hatua inayosababisha kufika shuleni kwa kuchelewa na kusababisha ongezeko la matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo kubakwa ama kulawitiwa.

Amesema watoto wanatoka Mtaa wa Kanenwa uliopo Kata ya Kishiri kwenda shule ya Bukaga umbali wa kilomita 2.5 na wengine wanaenda shule ya Bujingwa ambapo wanatumia kilomita 3.5 hivyo kuwepo na shule katika Mtaa huo kutasaidia kupunguza adha kwa wanafunzi kwenda kufuata masomo umbali mrefu.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Luchelele, Vicent Tegge amesema Kata ya hiyo ina shule mbili za sekondari na kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi kuna umuhimu wa kuongeza Sekondari nyingine ambapo wananchi wapo tayari kuchangia ujenzi huo na kwamba eneo lipo Mtaa wa Kisoko ila changamoto ni kulipa fidia ya ardhi.

"Waziri wa ardhi, Angelina Mabula alilitembelea eneo la Mtaa wa Kisoko Okutoba 27, 2021 na aliahidi malipo ya fidia kufanyika kabla ya mwaka wa fedha kumalizika" amesema Tegge.

Ameongezwa kwamba kuna changamoto nyingine nyingi ambazo alishaziwasilisha kwenye mabaraza hadi sasa zina miaka 7 hazijapatiwa ufumbuzi na kuhimiza hatua za utekelezaji kuchukuliwa.

Naye Mussa Ngolo ambaye ni diwani wa Kata ya Igoma amesema Kituo cha afya Igoma hakina Genereta, mochwari, mashine ya X-ray, vifaa tiba pamoja na uhaba wa watumishi hivyo ni vyema Serikali ikatatua changamoto hizo ili jamii iendelee kupata huduma bora za afya.

Akizungumzia upande wa eneo la mazishi, Ngolo amesema Igoma pamejaa hivyo anaiomba Halmashauri ya Jiji la Mwanza iruhusu eneo ambalo liko Kanindo lianze kutumika kwa ajili ya mazishi.

Kwa upande wake Diwani Kata ya Nyegezi, Edith Mudogo amesema barabara ya Kuzenza kwenye makutano ya barabara ya Sauti ni mbovu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha zinazidi kuharibu zaidi hivyo kuomba ufanyiwe ukarabati.

Kaimu Mkurugenzi wa Halimashauri ya Jiji la Mwanza, Orcado Grayson ameeleza kupotea ushauri huo wa madiwani na kuzifikisha katika ngazi ya maamuzi kwa ajili ya hatua za utekelezaji kuchukuliwa.

1 comment:

  1. Begin your betting journey with our turnkey Sportegrator platform, powered by customizable software program and broad range|a variety} of sports activities knowledge feeds. While bonuses can draw gamers in, you’ll 우리카지노 want different strategies to retain them. Initial investment and operating prices will differ throughout markets, so the amount of capital may have} readily available could have a big affect on your decision.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.