LIVE STREAM ADS

Header Ads

Walimu Nyamagana wamwangukia Rais Samia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Jukwaa la Walimu Wazalendo Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza limeiomba Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya walimu kufanyia kazi hususani ujenzi wa nyumba za walimu, posho za kujikimu katika mazingira magumu ikiwemo visiwani ama vijijini kusipokuwa na miundombinu rafiki.

Katibu wa Jukwaa hilo, Mwl. Emmanuel Masanja ametoa ombi hilo Juni 03, 2022 jijini Mwanza wakati akitoa tamko la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa utendaji kazi wake tangu aingie madarakani.

Mwl. Masanja amesema walimu wanampongeza Rais Samia kwa kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kwa asilimia 23.3, kuwalipa watumishi elfu 65 madai yao kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 90, ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia fedha za Uviko 19 pamoja na kutangaza vivutio vya utalii nchini kupitia filamu ya Royal Tour.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Viongozi wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Wilaya Nyamagana wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Katibu wa Jukwaa la Waalimu Wazalendo Wilaya ya Nyamagana, mwl. Emmanuel Masanja (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Mwl. Leticia Sitta (kulia) wakati wakitoa tamko la kumpongeza Rais Samia.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.