LIVE STREAM ADS

Header Ads

Askofu Kasala alia na mzigo wa kodi taasisi za dini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Geita, Flavian Kasala ameiomba Serikali kutafakari upya na kuondoa mzigo wa kodi uliopo kwenye taasisi za elimu zinazomilikiwa na madhehebu ya dini kwani taasisi hiyo hazifanyi biashara.

Aliyasema hayo Jumanne Juni 07, 2022 wakati akizungumza kwenye Ibada Maalum Kumuombea Mwasisi wa Taasisi ya St. Caroli iliyopo Sengerema mkoani Mwanza, Sr. Tarsicius Heijmink ambaye alikuwa rai wa Uholanzi.

Askofu Kasala alisema taasisi za elimu zinazomilikiwa na dini ikiwemo shule na vyuo kwa asilimia kubwa zinaendeshwa kwa misaada ya wafadhili mbalimbali hivyo hatua ya kutakiwa kulipa kodi inazinyima fchangamoto ya kujiendesha.

Katika Misa hiyo, pia Askofu Kasala aliongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika Shule ya Msingi St. Caroli ambapo zaidi ya shilingi milioni 20 zilipatikana ikiwa ni ahadi na fedha tasilimu.

Mkuu wa taasisi ya St. Caroly, Glory Samba alisema makadirio ya ujenzi wa bweni hilo ni shilingi milioni 70 hadi kukamilika na hivyo kuwaomba wadau wa elimu wakiwemo wazazi kuchangia ili kukamilisha ujenzi huo na kuwaondolea adhani wanafunzi.

Sr. Tarsicius Heijmink alizaliwa Januari 19, 1925 na kufariki dunia Mei 22, 2022 akiwa na miaka 97 ambapo taasisi ya St. Caroli aliyoianzisha inaendesha shule za mchepuo wa kiingereza (English Medium) za Awali, Chekeches, Msingi na Sekondari mjini Sengerema.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Geita, Flavian Kasala akizungumza kwenye misa hiyo ya kumuombea Sr. Tarsicius Heijmink ambapo aliwasihi waumini wa Kanisa Katoliki hususani jamii ya Sengerema kuyaishi matendo mema mema ya Sr. Tarsicius Heijmink na pia kuwa na siku maalum ya kufanya kumbukizi yake kila mwaka.
Mwal. John Chamika ambaye ni miongoni mwa waalimu wa kwanza walioanza kufanya kazi Shule ya Msingi St. Caroli wakati inaanzishwa mwaka 1995 akieleza namna Sr. Tarsicius Heijmink alifanya jitihada kubwa kutoa maarifa ya elimu kwa jamii ya watu wa Sengerema na kuhimiza watu kuyaenzi mema yote aliyowaachia.
Mmoja wa watoto waliokuwa wakilelewa na Sr. Tarsicius Heijmink akieleza namna alivyowasaidia watoto wengi kupata elimu.
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Geita, Flavian Kasala akiongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa bweni kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Msingi St. Caroli.
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Geita, Flavian Kasala akiongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa bweni kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Msingi St. Caroli.
Harambee ikiendelea...
Washiriki kutoka maeneo mbalimbali wakishiriki harambee hiyo.
Harambee ikiendelea.
Masista wakichangia harambee hiyo.
Mkuu wa taasisi ya St. Caroli, Sr. Glory Samba (kushoto) akiwabidhi keki wanafunzi waliosoma kwenye shule hiyo baaada ya kushiriki harambee.
Mkuu wa taasisi ya St. Caroli, Sr. Glory Samba (kushoto) akiwabidhi keki wanafunzi waliosoma kwenye shule hiyo baaada ya kushiriki harambee.
Wanafunzi nao walishiriki harambee hiyo.
Wanafunzi wa St. Caroli wakishiriki harambee hiyo.
Wanafunzi waliokuwa wakilelewa na Sr. Tarsicius Heijmink wakiwa kwenye misa hiyo.
Wanafunzi waliokuwa wakilelewa na Sr. Tarsicius Heijmink wakiwa kwenye misa hiyo.
Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Yesu Kristo Mfalme mjini Sengerema, Jimbo Kuu la Geita wakipokea mkate wa uzima.
Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Yesu Kristo Mfalme mjini Sengerema wakipokea mkate wa uzima.
Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Yesu Kristo Mfalme mjini Sengerema wakipokea mkate wa uzima.
Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Yesu Kristo Mfalme mjini Sengerema wakipokea mkate wa uzima.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari St. Caroli wakiimba wakati wa misa.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari St. Caroli wakiimba wakati wa misa.
Misa ikiendelea.
Waumini wakifuatilia misa hiyo.
Waumini wakiwa kwenye misa hiyo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.