LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbio za 'Mwanza Night Run' kufanyika mwezi Julai

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Salum Kalli akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwaza Night Run.
Mwanachama wa Klabu ya riadha ya Rock City Runners, Magreth Mushi akisoma risala ya uzinduzi wa mbio za Mwaza Night Run.
Katibu wa Klabu ya Rock City Runners, Idd Zubery akielezea njia zitakazotumika wakati wa mbio za Mwanza Night Run.
Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza, Julius Kambarage akizungumza kwenye uzinduzi wa mbio za Mwaza Night Run.

Picha ya pamoja
***

Na Hellen Mtereko, Mwanza
Klabu ya Riadha ya Rock City Runners imezindua mbio ya Mwanza Night Run kwa lengo la kujenga uelewa kwa jamii kuhusiana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mbio hizo zenye kilometa saba na kilometa 15 zinatarajia kufanyika Julai 23, 2022 zikiwa na kauli mbiu isemayo "Wajibu wa Kuimarisha Ulinzi na Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ni Wetu Sote, Jiandae Kuhesabiwa".

Akisoma risala wakati wa ufunguzi wa mbio hizo, mmoja wa wanachama wa Klabu ya Rock City Runners, Magreti Mushi alisema Mwanza Nigh Run ni mbio za kwanza kufanyika katika Mkoa wa Mwanza na lengo kubwa ni kuwaleta watu pamoja kukimbia ili kupaza sauti ya kuimarisha ulinzi na kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Alisema klabu hiyo imeandaa programu ijulikanayo kama "tumeamua ukatili sasa basi" katika shule na vyuo mkoani Mwanza kwa lengo la kutoa elimu kwa wanafunzi ili kukuza uelewa wa namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kagemlo Muhula kutoka dawati la jinsia jeshi la polisi Wilaya ya Nyamagana, aliishukuru klabu hiyo kwa kuandaa mbio zitakazo hamasisha jamii kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuongeza kuwa ukatili ni jambo ambalo limekuwa likiathiri akili za watu wengi, hivyo kupitia mbio hizo jamii itaamka na kuona kwamba ukatili haukubaliki.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza, Julius Kambarage alieleza kuwa mbio ni sehemu ya mazoezi na zinasaidia kuweka akili sawa na kupunguza fikira potofu zinazochochea vitendo vya ukatili.

Pia ametoa rai kwa jamii kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo zitakazosaidia kutoa elimu kwa wananchi kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto.

Awali akizindua mbio hizo, Mkuu wa Wilaya ya Magu Salumu Kalli alihimiza zikawe chachu kwa jamii na kuleta matokea chanya ambayo yatasaidia kupunguza au kumaliza kabisa ukatili kwa wanawake na watoto katika Mkoa wa Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.