LIVE STREAM ADS

Header Ads

Filamu ya 'Tanzania The Royal Tour' kutambulishwa Mwanza kwa kishindo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wananchi na wadau mbalimbali wa utalii wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia filamu ya 'Tanzania, The Royal Tour' inayotarajiwa kutambulishwa jijini Mwanza.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel ametoa ombi hilo Juni 11, 2022 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na utambulisho wa filamu hiyo unaotarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya elfu moja.

Mhandisi Gabriel amesema kwa Mkoa Mwanza, filamu ya 'Tanzania, The Royal Tour itatambulishwa siku ya jumamosi Juni 18, 2022 katika eneo la Rock City Mall kuanzia majira ya saa tisa alasiri.

Amesema kuzinduliwa kwa filamu hiyo iliyochezwa na Rais Samia Suluhu Hassan kumesaidia kuvitangaza kimataifa vivutio vya utalii nchini na hivyo kuongeza idadi ya watalii ambao pia watasaidia pato la taifa kuongezeka.

Amesema kuelekea kwenye utambulisho wa filamu ya Tanzania, The Royal Tour mkoani Mwanza, wananchi na wadau mbalimbali watatembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Juni 16, 2022) na vivutio vya utalii vilivyopo jijini Mwanza (Juni 17, 2022).

Kwa upande wao, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa Cha Saanane, Eva Malya na Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Gloria Munhambo wamesema wamejiandaa kuwapokea na kuwahudumia watalii wa ndani na nje ya nchi baada ya idadi yao kuongezeka kutokana na filamu ya 'Tanzania, The Royal Tour'.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza kuhusiana na utambulisho wa filamu ya Tanzania The Royal Tour jijini Mwanza.
Waandishi wa habari jijini Mwanza wakinasa matukio.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kuelekea kweye utambulisho wa filamu ya Tanzania The Royal Tour unaotarajiwa kufanyika jumamosi Juni 18, 2022 Rock City Mall kuanzia majira ya saa tia alasili.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa Cha Saanane, Eva Malya (kulia) na Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Gloria Munhambo (katikati) wakifuatilia mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali utalii mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa Cha Saanane, Eva Malya (kushoto).
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa, Gloria Munhambo
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari jijini Mwanza ambao ni wadau muhimu wa kutangaza vivutio vya utalii nchini.

No comments:

Powered by Blogger.