LIVE STREAM ADS

Header Ads

Bwiru Girls yapiga marufuku ufaulu wa daraja la tatu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Bwiru Wasichana iliyopo Ilemela mkoani Mwanza, wakila kiapo cha kusoma kwa bidii ili kufaulu kwa daraja la kwanza na la pili pekee katika mtihano wao wa mwisho mwakani 2023.

Wamekula kiapo hiki wakati wa hafla ya kuipongesha Shule hii baada ya kufanikiwa kuondoa ufaulu wa daraja la nne katika mtihani wa kidato cha sita mwaka huu 2022 ambapo itakumbukwa shule hii ya Bwiru wasichana ilifanikiwa kuondoa ziro miaka mitatu iliyopita.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwiru Wasichana, Mwl. Mecktrida Shija (kulia) akipokea zawadi ya motisha baada ya Shule hiyo kufanikiwa kuondoa ufaulu wa daraja la nne pamoja na ziro katika matokeo ya kidato cha sita.
Mmoja wa wanafunzi wa kidato cha sita Shule ya Sekondari Bwiru Wasichana akipokea zawadi baada ya kufanya vizuri katika mitihani ya majaribio kabla ya kuelekea kwenye mtihani wa mwisho wa kitaifa.
Naibu Meya Manispaa ya Ilemela, Manusura Lusigaliye akizungumza kwenye hafla ya kuipongeza Shule ya Sekondari Bwiru Wasichana baada ya kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka huu 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akitoa salamu kwenye hafla hiyo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.