LIVE STREAM ADS

Header Ads

Chuo Kikuu SAUT kuanza kutoa kozi ya Usafiri wa Anga/ Aviaton

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) ndaki ya Mwanza kinatarajia kuanza kutoa mafunzo ya usafiri wa anga ili kuwawezesha wahitimu wake kunufaika na fursa mbalimbali za ajira zilizopo katika sekta hiyo.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Costa Ricky Mahalu ameyasema hayo Juali 29, 2022 wakati za zoezi la kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya SAUT na Chuo cha usafiri wa anga cha Regional Aviation & Business kilichopo kilichopo Dar es salaam.

Prof. Mahalu amesema makubaliano hayo ya miaka mitano yatasaidia wanafunzi wa Chuo Kikuu SAUT kubadilishana uzoefu hususani mafunzo kwa vitendo baada ya kuhitimu mafunzo ya nadharia katika nyanja mbalimbali zinazohusiana na usafiri wa anga.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Regional Aviation, Capt. Phillemon Kisumo amesema mwamko wa watanzania kunufaika na fursa za usafiri wa anga bado ni mdogo hivyo ushirikiano baina ya Chuo chake na Chuo Kikuu SAUT utakuwa na manufaa makubwa.

Inelezwa kuwa Tanzania imeanza kupiga hatua katika usafiri wa anga hususani baada ya kuimarisha utendaji kazi wa Shirika la ndege ATCL ikiwemo kuongeza idadi ya ndege mpya na hivyo kufanya sekta hiyo kuchocheo ukuaji wa uchumi kwa watanzania.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Prof. Costa Ricky Mahalu (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Regional Aviation & Business, Cpt. Phillemon Kisumo (kushoto) wakisaini makubaliano ya ushirikiano.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Prof. Costa Ricky Mahalu (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Regional Aviation & Business, Cpt. Phillemon Kisumo (kushoto) wakionyesha hati za makubaliano.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.