LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kombe la Utalii kurindima jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA) kwa kushirikiana na kampuni ya FRAKI inayojihusha na sanaa, michezo na utalii wameandaa michuano ya Kombe la Utalii (Utalii Cup) 2022 itakayofanyika jijini Mwanza.

Katibu Mkuu MZFA, Mwl  Leonard Malongo (kushoto) amesema michuano hiyo inalenga kuhamasisha na kuendeleza vipaji vya wachezaji, kutoa nafasi kwa timu za mikoa ya Kanda ya Ziwa kupata fursa ya kujiandaa kabla ya msimu wa ligi kuanza pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani.

Malongo amesema michuano hiyo kwa msimu huu inatarajia kuanza Julai 27, 2022 na kumalizika Agositi 12, 2022 huku akisema dhamira yao kubwa ni kufanya kombe la utalii kuwa endelevu.

Kwa upande wa zawadi Malongo amesema mshindi wa kwanza atapata shilingi milioni tano, kombe na medali, mshindi wa pili atapata shilingi milioni tatu na medali, mshindi wa tatu atapata milioni moja na laki tano huku mahindi wa nne akipata shilingi laki tano.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya FRAKI, Francis Shao (katikati) amesema kombe la utalii litasaidia kuhamasisha jamii kuenzi sanaa, tamaduni pamoja na kukusanya michango ya Fedha kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya Shule mbalimbali jijini Mwanza.
Naye Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi kutoka Kisiwa cha Saanane, Eva Malia (katikati) amesema utalii wa michezo ni utalii ambao umeshika kasi duniani hivyo kombe hilo litachochea ukuaji wa sekta ya utalii Kanda ya Ziwa.

Malia ametoa wito kwa timu za soka zitakazoshiriki mashindano hayo pamoja na mashabiki kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo jijini mwanza ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane.
Na Hellen Mtereko, Mwanza 

No comments:

Powered by Blogger.