LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mahafali ya 10 Chuo Cha Afya Kolandoto Shinyanga yafana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga wakiandamana kutoka jengo la Utawala la Chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali yao ya 10 yaliyofanyika chuoni hapo.
Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi Kolandoto Manispaa ya Shinyanga yamefanyika Ijumaa Julai 29,2022 ambapo jumla ya wanafunzi 255 wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’.

Mgeni rasmi katika Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kinachomilikiwa na Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) alikuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Masumbuko alikipongeza Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kwa kutoa Programu mbalimbali na kuanza mchakato wa kuanzisha Chuo Kikuu cha Kolandoto akisema ni mipango ya mkoa wa Shinyanga kuanzisha vyuo mbalimbali mkoani humo ili kuongeza fursa za kiuchumi.

“Serikali ya mkoa wa Shinyanga inaendelea kuvutia wawekezaji mbalimbali ili wawekeze katika vyuo ili kuubadilisha mkoa wa Shinyanga…Ni fursa kwenu kuchangamkia fursa ya elimu ya juu sisi mkoa tumejipanga kufanikisha haya” alisema.

“Serikali imeridhia kutoa sehemu ya eneo la shule ya Msingi Kolandoto ili kuongeza eneo la chuo cha Kolandoto" alisema Masumbuko.

Aidha amewataka wahitimu hao kwenda kuzingatia maadili pindi watakapoanza kuhudumia wananchi katika jamii.

“Elimu hii mliyopata ni elimu kubwa na sasa mnaenda kuingia katika ulimwengu wa kiutendaji, mnapaswa kwenda kuwa chachu, mkawe waadilifu mnapohudumia wananchi, mavazi yenu yakawe mazuri, lugha nzuri, na mkajiendeleze kielimu pia, elimu za juu zitawapa fursa zaidi za ajira” alisema Masumbuko.

Akisoma taarifa ya chuo hicho, Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Dkt. Paschal Shiluka alisema jumla ya wahitimu wa kozi mbalimbali mwaka huu ni 255 kati yao 139 ni wa jinsia ya kike akibainisha kuwa lengo la chuo ni kuwa na 50% kwa 50% na wamevuka lengo la serikali kwa kuwa na wanafunzi wa jinsia ya kike zaidi ya 50%.

Alisema Wanafunzi 255 wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga ‘Nursingi and Midwifery’, Maabara ya Binadamu ‘Medical Laboratory Sciences’, Utabibu ‘ Clinical Medicine’, Ufamasia ‘Pharmaceutical Sciences’, na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’ ambazo zinaotolewa na Chuo cha Sayansi za Afya kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).

“Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kilianzishwa mwaka 1957 kikiwa na Programu moja na sasa kimekuwa na ongezeko la Programu na wanafunzi kila mwaka, wahitimu wa kwanza walikuwa sita tu tofauti na tunaposherehekea mahafali haya ya 10 tukiwa na wahitimu 255” alisema Dkt. Shiluka.

“Upekee wa mahafali ya mwaka huu, kwanza mahafali haya yameanza kwa kuwa na wiki la Mahafali ambapo kwa kushirikiana na Shirika la Doctors with Africa tumeweza kutoa huduma za afya kwa jamii na wanachuo, jumla ya wananchi 75 wamepatiwa chanjo ya Uviko 19, 100 wamepima magonjwa yasiyoambukiza, hali kadhalika kumwe na michezo mbalimbali iliyoshirikisha wanafunzi,wataaluma na wafanyakazi wa Chuo na Hospitali” alieeeleza.

Aliwataka wahitimu hao kuondokana na imani potofu ya kusubiri ajira kutoka serikalini kwani ujuzi waliopata chuoni unawezesha wao kujiajiri na kuajiri wengine.

“Mawazo ya kusubiri ajira serikalini ni mawazo potofu. Changamoto zilizopo katika jamii mzitumie kama fursa ya kujiajiri na kuajiri wengine, utaalamu mliopata chuoni utumieni kujiajiri na kuajiri wengine, nendeni mkaanzishe maabara zenu, famasi zenu na taasisi zingine kwa kadri Mungu atakavyowajalia” aliongeza Dkt. Shiluka.

“Tunaendelea na utekelezaji wa Mpango mkakati wa miaka mitano ukiwa na malengo ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Kolandoto (-Kolandoto University - KOU) ifikapo mwaka 2026,kubaini, kupima ardhi na kuweka uzio katika maeneo yote ya chuo, kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza katika miundo mbinu wezeshi kwenye uanzishwaji wa Chuo Kikuu, kuwa na mpango rasmi (Land Master Plan) wa ardhi na kuwa na wanachuo zaidi ya 3000” alisema Dkt. Shiluka.

Aliongeza kuwa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto kimekuwa na mafanikio mengi ikiwemo kupanua na kukarabati maabara ya kufundishia na kuweza kutumiwa na wanafunzi 100 kwa wakati mmoja, kujenga kumbi mbili za madarasa, kupanua maktaba ya chuo,kuongeza kozi ya utabibu katika Kampasi ya Mwanza, kukarabati nyumba 2 za watumishi,kukarabati hosteli 2,kuboresha maslahi na motisha kwa watumishi,kujenga vimbweta, kushiriki Maonesho ya kitaifa ya vyuo vya kati na vyuo vikuu Dodoma na kupeleka watumishi wake kwenye hifadhi ya taifa ya Ruaha.

Aidha aliomba eneo la Kolandoto liwe na kituo cha polisi na kuhamasisha uwekezaji wa nyumba za makazi eneo la chuo kwa kujenga Hosteli za wanafunzi na kuongeza huduma za kijamii.

Naye Askofu Mkuu Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota aliwataka wahitimu hao watakapokwenda kuanza kufanya kazi wazingatie maadili ya kazi yao huku akiwashauri kutumia elimu waliyopata kusaidia jamii.
Na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiandamana kutoka Jengo la Utawala la chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali yao 10. 
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiandamana kutoka Jengo la Utawala la chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiandamana kutoka Jengo la Utawala la chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiandamana kutoka Jengo la Utawala la chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiandamana kutoka Jengo la Utawala la chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiandamana kutoka Jengo la Utawala la chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kwenye Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Dkt. Paschal Shiluka akizungumza kwenye Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Askofu Mkuu Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota akizungumza kwenye Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Idara ya Afya wa Kanisa la AICT Dkt. Leopord Gilala akizungumza kwenye Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Mch. Juma Kiyumbi akizungumza kwenye Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Wahitimu wa Programu ya Ukunga na Uuguzi wakiwa kwenye Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiwa kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Wazazi na wageni wakiwa kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Wazazi wakiwa kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
AICT Tumaini Choir ikitoa burudani kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mhitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto akitoa burudani kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto. Wahitimu hao wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiwatunuku Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mahafali yanaendelea.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto. Wahitimu hao wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto. Wahitimu hao wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto. Wahitimu hao wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto. Wahitimu hao wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto. Wahitimu hao wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Wahitimu wa Programu ya Uuguzi na Ukunga wakila kiapo.
Wahitimu wa Programu ya Maabara wakila kiapo.
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakipiga picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi.

No comments:

Powered by Blogger.