LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Nyamagana awasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Juni 2022.

Makilagi amewasilisha taarifa hiyo, Jumamosi Agositi 13, 2022 mbele ya wajumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Nyamagana na kueleza kuwa miongoni mwa mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi hicho ni pamoja na kuboresha sekta ya kilimo.

Amesema kumekuwa na mageuzi makubwa katika sekta hiyo na sasa wakulima wanazingatia kilimo cha kisasa, kibiashara na chenye tija baada ya kuwatembelea na kuwashauri wakulima hususani wa mbogamboga, matunda na mazao ya chakula kupitia kwa maafisa ugani wapatao 15.

"Jumla ya Kata 12 zimetembelewa na kupewa ushauri wa ugani, pia maduka 58 ya uuzaji wa pembejeo yalikaguliwa ili kuweza kujiridhisha na kile wanachokiuza kama ni salama kwa matumizi ya kilimo chenye tija" alisema Makilagi.

Alieleza kuwa kupitia mfumo wa kilimo (M-Kilimo) kwa kipindi cha Juni 2022 jumla ya wakulima na wadau wa kilimo 3,541 walisajiliwa katika Wilaya ya Nyamagana huku akisema usajili bado unaendelea.

"Mfumo wa M-Kilimo ni kwa ajili ya kuwasajili wakulima, pia ni njia rahisi ya mawasiliano kati ya mtaalamu wa ugani na mkulima katika kutoa ushauri wa kilimo na upatikanaji wa masoko ya bidhaa za kilimo" alisema Makilagi.

Wajumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Nyamagana wameeleza kuridhishwa na taarifa hiyo huku pia wakimpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyotoa fedha za kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo ya kimkakati mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25 katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Juni 2022. Taarifa hiyo imeangazia mafanikio katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, elimu, miundombinu, kilimo na ufugaji.
Awali Mwenyekiti CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athumani akiwahimiza viongozi wa chama hicho waluochaguliwa katika nafasi mbalimbali kufanya kazi kwa ukaribu na wananchi, kusikiliza kero zao na kuzishughulikia kwa wakati.
Wajumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Nyamagana wakifuatilia mkutano huo.
Na Hellen Mtereko, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.