LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waalimu wampongeza Rais Samia kwa nyongeza ya mishahara na upandishaji madaraja

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Chama cha Walimu (CWT) Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kimempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Haasan kwa kuendelea kuwajali watumishi wa kada hiyo kwa nyongeza ya asilimia 23 kwa wafanyakazi wa kima cha chini cha mshahara pamoja na upandishaji wa madaraja.
Mwenyekiti wa (CWT) wilayani Nyamagana, Mwal. Sholi Maduhu amesema ameamua kutoa pongezi hizo ikiwa ni kutambua mchango wa Mhe.Rais Samia wa kuwa msikivu nakuendelea kutatua kero sugu ambazo wameishi nazo kwa kipindi cha miaka saba.

"Tunasema haya kwa kuwa watanzania tumekuwa wepesi wa kusahahu lakini lazima tuseme haya Mhe.Rais alihaidi mara tu alipoingia madarakani na tumeanza kuona matunda yake wa kipindi kifupi cha uongozi wake akiwa ofisini kwa takribani mwaka mmoja na nusu tu" amesema Maduhu.

Mwal. Maduhu amesema kuwa mbali na nyongeza ya mshahara lakini pia watumishi wamepandishwa madaraja na mishahara yao imepanda kitu ambacho huko nyuma walisahau.

Aidha Maduhu amemuomba Mhe. Rais kukemea wafanyabishara ambao wamezidi kupandisha gharama za maisha kwa maana ya bidhaa mara tu baada ya kusikia watumishi wamepandishwa mishahara.

"Tunalaani kitendo cha wafanyabishara kupandisha bidhaa holela kinyume na taratibu kiwa na kuwasihi wafanyabiashara wawe wazalendo wa nchi yao" amesisitiza.

Kwa Upande wake Mwal. Raymond Ogowa Mwakilishi wa Walimu wenye ulemavu amempongeza Mhe.Rais kwa kuendelea kuwajali watumishi wenye uhitaji maalum kwa kuwezesha taasisi za mikopo kuwakopesha na kuwa na na unafuu wa maisha.

Ogowa pia amemuomba Mhe.Rais Samia kuendelea kuimarisha ulinzi kwa ajili ya watanzania wote ili kuendela kulinda amani ambayo tuliachiwa na waasisi wetu.

Naye Mwalimu Veronica Haule amempongeza Mhe.Rais kwa kuendela kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa kuongeza vyumba vya madarasa jambo ambalo linazidi kuongeza ufanisi kwa wanafunzi pamoja na walimu wao.
Na Oscar Mihayo, Mwanza 

No comments:

Powered by Blogger.