LIVE STREAM ADS

Header Ads

Hamasa ya Sensa yapamba moto Nyamagana, DC ateta na wananchi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi uliofanyika jijini Mwanza.
***

Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wananchi katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wametakiwa kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agositi 23, 2022.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi alitoa rai hiyo Agosti 18, 2022 wakati Akizungumza kwenye mkutano wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita wilayani humo, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na uhamasishaji wanachi kuwa tayari kushiriki kwenye zoezi la Sensa.

Makilagi aliwaeleza wananchi umuhimu wa kushiriki Sensa kwani itasaidia Serikali kupata takwimu sahihi za idadi ya watu na kuwapangia mipango ya maendeleo inayoendana na uhalisia.

"Sensa inaisaidia Serikali kupata idadi ya watoto, wazee, vijana, wanawake, wanaume, walemavu na wenye mahitaji maalumu hivyo kila mtu anatakiwa kuhesabiwa. Niwaombe sana muwe wakweli kwenye kutoa taarifa za idadi ya watu wanaoishi kwenye familia zenu" alihimiza Makilagi.

Naye Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula aliwaasa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye Sensa ya Watu na Makazi ili kuisaidia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazowezesha mchakato wa utekelezaji wa dira ya maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi katika sekta ya afya pamoja na utekelezaji wa ajenda mbalimbali za maendeleo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi walioshiriki kwenye mkutano huo uliofanyika eneo la mnara wa Nyerere jijini Mwanza walisema wako tayari kushirikiana vyema na makarani wa Sensa ili kufanikisha zoezi hilo.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi akihamasisha wananchi kutoka ushirikiano kwa Makarani ili kufanikisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi, Agosti 23, 2022. 
Viongozi mbalimbali wilayani Nyamagana wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Amina Makilagi (wa tatu kushoto) wakiwa kwenye mkutano wa kuhamasisha wanachi kuwa tayari kushiriki Sensa ya Watu na Makazi, Agosti 23, 2022.
Ratiba ya mikutano ya Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi yenye lengo la kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi, kumsikiliza na kutatua changamoto zao pamoja na kuwahimiza kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi, Agosti 23, 2022.

No comments:

Powered by Blogger.