LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wazazi watajwa chanzo cha watoto kupata ugonjwa wa maskio

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Imeelezwa kuwa tatizo la ugonjwa wa masikio kwa watoto wadogo linasababishwa na wazazi kuchelewa kuwapeleka watoto hospitali ili kufanyiwa uchunguzi wa kupima usikivu wao.

Kauli hiyo imetolewa na Halima Shamsi ambaye ni Mtaalamu wa usikivu kutoka hospitali ya rufaa ya Bugando wakati akizungumzia tatizo la usikivu kwa watu wazima na watoto wadogo.

Halima alisema watu wengi hupata tatizo la usikivu wakiwa watoto kutokana na wazazi wengi hujishindwa kugundua mapema tatizo hilo la usikivu hadi pale mtoto anapokuwa mtu mzima na kusababisha ugonjwa kukua.

"Upande wa ugonjwa wa masikio hivi sasa wagonjwa ni wengi sana na wengi wanatembea wakiwa hawajui wanasikia katika kiwango gani na wale wanaokuja hospitali tayari wanakuwa wamechelewa" alisema Halima.

Halima aliwataka wazazi kuhakikisha wanawafanyia uchunguzi watoto wao kabla ya kufikisha umri wa miaka 10 ili waweze kusaidiwa mapema kuwa na usikivu mzuri kama ilivyo kwa Watoto wengine.

Alizitaja dalili za mtoto mwenye tatizo la usikivu kuwa ni pamoja na mtoto anajitenga,kutogeuka kufuata milio ya vitu pamoja pamoja na kuchelewa kuongea.
Halima alisema kwa sasa hospitali ya rufaa ya Bugando inatoa matibabu ya matatizo hayo ya usikivu kwa kufanya uchunguzi ili kujua aina ya matibabu ambayo mgonjwa anatakiwa kupatiwa.

"Kwa watoto ambao tukiwapima na kuwakuta usikivu wao umeshuka kuna vifaa ambavyo tunawapatia vya kuwasaidia waweze kusikia vizuri na wale ambao wanakuwa na tatizo kubwa wakati mwingine huwa tunawafanyia upasuaji" alisema Halima.

Aliwata wazazi ambao watoto wao wamepatwa na tatizo la kutosikia kabisa kuhakikisha wanawaendeleza kielimu kwa kuwapeleka shule zenye Watoto wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata haki ya kupata elimu.

Serikali ya Tanzania kupitia sera ya afya 2007 imewekeza sana katika kuboresha uhai wa mtoto kupitia utoaji wa huduma bure za afya kwa kina mama wajawazito na Watoto chini ya miaka 5.
Na Tonny Alphonce, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.