LIVE STREAM ADS

Header Ads

Upungufu wa umeme kubaki historia, TANESCO yawatoa hofu wateja

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja TANESCO, Martine Mwambene amewatoa hofu wateja wa shirika hilo kwamba changamoto ya upungufu wa umeme nchini itabaki historia baada ya kukamilika kwa miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na shirika hilo.

Mwambene aliyasema hayo Jumanne Oktoba 04, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Wiki ya Huduma kwa Wateja 2022 ambapo aliongeza kuwa shirika hilo pia linatarajia kuanza utekelezaji wa miradi mipya ya umeme itakayosaidia kuimarisha hali ya upatikanaji wa nishati hiyo.

Naye Meneja wa TANESCO Mkoa Mwanza, Mhandisi Said Msemo alisema shirika hilo linatarajia kujenga kituo cha kupooza na kusambaza umeme katika eneo la Usagara ili kusaidiana na vituo vya Nyakato na Mabuki hatua itakayoondoa changamoto ya kukatika umeme ambayo kwa sasa inasababishwa na miundombinu kuelemewa na si upungufu wa umeme kwani mahitaji yaliyopo ni kidogo ikilinganishwa na uzalishaji uliopo.
Tazama BMG TV hapa chini
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

No comments:

Powered by Blogger.