LIVE STREAM ADS

Header Ads

TANESCO Mwanza wawaibukia wateja wakubwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani, maafisa wa shirika la TANESCO Mkoa Mwanza wamewatembelea wateja wakubwa wa shirika hilo ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao na kuimarisha ushirikiano.

Zoezi la kuwatembelea wateja hao lilifanyika jumanne Oktoba 04, 2022 ambapo miongoni mwa wateja waliobahatika kupata fursa hiyo ni kiwanda cha samaki Nature’s, kiwanda cha nondo Nyakato, kiwanda cha kuzalisha soda Nyanza pamoja na kiwanda cha kuzalisha hewa ya Oksijeni cha O2 Limited.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililoambatana na ugawaji wa zawadi ikiwemo vikombe na kofia zenye nembo ya TANESCO, Afisa Masoko wa shirika hilo Mkoa Mwanza Prisca Kayaga alisema hatua hiyo inasaidia pia kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wateja utakaosaidia shirika kuboresha huduma na kuwahudumia kulingana na mahitaji yao.

Naye Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Joyce Makori aliwatoa hofu wateja hao kwamba shirika linaendelea kuboresha huduma zake, kutekeleza miradi mikubwa ya kuzalisha umeme ikiwemo Mwalimu Nyerere na Rusumo ambayo baada ya kukamilika itasaidia kutatua changamoto ya upungufu wa umeme nchini.

Nao wateja akiwemo Meneja kampuni ya Nyanza, Peter Simon pamoja na Mkurugenzi Mtendaji kiwanda cha O2, Abul Kalam waliomba TANESCO kuendelea kuimarisha mawasiliano kwa wateja wake hususani inapotokea dharura ya ukosefu wa umeme hatua inayowasaidia kupanga vyema ratiba ya uzalishaji.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Maafisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga (kulia) na Joyce Makori (kushoto) wakiwa na Meneja kiwanda cha Nyanza Botlling Company Limited, Peter Simon (katikati) baada ya kumtembelea ofisini kwake.
Maafisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga (kulia) na Joyce Makori (katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa kiwanda cha Nature's Fish, Ronald Pereira (kushoto) baada ya kumtembelea kiwandani hapo. 
Maafisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga (kulia) na Joyce Makori (katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Mkuu kiwanda cha Nyakato Steel Mills (kushoto).
Maafisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga (kulia) na Joyce Makori (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Fedha kiwanda cha Nyakato Steel Mills, Prabhakar Botlagunta (kushoto) na Meneja Mkuu wa kiwanda hicho (wa pili kulia).
Maafisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga (kulia) na Joyce Makori (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kutembelea kiwanda cha nondo Nyakato.
Maafisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga (kulia) na Joyce Makori (kushoto) wakizungumza na Mkurugenzi Mtendaji kiwanda cha Oksijeni cha O2 Limited, Abul Kalam (wa pili kushoto). Wa pili kulia ni HR wa kampuni hiyo.
Maafisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga (kushoto) na Joyce Makori (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji kiwanda cha Oksijeni (O2 Limited), Abul Kalam (katikati).

No comments:

Powered by Blogger.