LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wahitimu mafunzo ya Mgambo Nyamagana wahimizwa uzalendo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi amehitimisha mafunzo ya awali ya askari wa Jeshi la Akiba (Mgambo) na kuwaasa wahitimu wa mafunzo hayo kuwa raia wema na kulitumikia Taifa kwa uadilifu.

Makilagi alifunga mafunzo hayo Ijumaa Novemba 04, 2022 katika uwanja wa Shule ya Msingi Iseni iliyopo Kata ya Butimba jijini Mwanza.

Alisema mafunzo hayo waliyoyapata yawe chachu ya kushiriki bila woga katika masuala yote ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Kwa upande wake Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Nyamagana, Meja Prisca Ishanju alisema mafunzo hayo yalianza Julai 04, 2022 ambapo jumla ya askari 93 wamehitimu ambapo kati yao askari wa kiume ni 81 na wa kike ni 12.

Meja Ishanju alisema matumaini ni wahitimu wa mafunzo hayo kuwa tegemeo kwenye maeneo wanayoishi kwa kuimarisha ulinzi ndani ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo, Husina Kakozi aliomba Serikali kuwapa kipaumbele katika ajira huku pia akiyaomba makampuni ya ulinzi kutoa mikataba ya ajira ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima kazini.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Kamanda Paredi, Boazi Nyoda (kushoto) akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi kukagua paredi ya wahitimu.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akikagua paredi ya wahitimu hao.
Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilayani Nyamagana wakila kiapo ya uadilifu.
Askari wa Jeshi la Akiba wilayani Nyamagana waliohitimu mafunzo yao ya awali.
Askari wa Jeshi la Akiba waliohitimu mafunzo ya awali wakipita kwa mwendo wa pole mbele ya mgeni wa heshima Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi (hayupo pichani).
Askari wa Jeshi la Akiba waliohitimu mafunzo ya awali wilayani Nyamagana wakipita kwa mwendo wa haraka.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilayani Nyamagana, Husina Kakozi (kushoto) akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake, kulia ni Adelina Adrian.
Christopher Batalinganya akiongoza bendi ya Jeshi la Akiba kwenye hafla ya kufungua mafunzo ya awali ya jeshi la akiba wilayani Nyamagana.
Mshauri wa Mgambo wilayani Nyamagana, Meja Prisca Ishanju akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya jeshi la akiba wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo 
Askari wa Jeshi la Akiba (mgambo) wakiwa kwenye hafla ya kuhitimi mafunzo yao wilayani Nyamagana.

No comments:

Powered by Blogger.