LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi wahimizwa kuwatumia watoa msaada wa kisheria kupata haki

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Imeelezwa kuwa ukosefu wa huduma za kisheria ni miongoni mwa changamoto inayowakwamisha wananchi kukosa haki katika mashauri mbalimbali yanayofikishwa kwenye vyombo vya utoaji haki ikiwemo mahakama.

Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kalii ameyasema hayo Novemba 05, 2022 wakati akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria na Siku ya Kujitolea duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.

Amebainisha kuwa wananchi wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya kisheria, wanashindwa kumudu gharama za kuwalipa mawakili na hivyo kushindwa kupata huduma wanapokumbwa na migogoro mbalimbali ikiwemo matukio ya ukatili wa kijinsia, migoro ya ardhi, ndoa na mirathi.

Kutokana na changamoto hiyo, Kalii amewahimiza wananchi kutambua umuhimu wa kupata ushauri wa kisheria kabla ya kuingia kwenye migogoro huku akivitaka pia vyombo vya usimamizi wa sheria na utoaji haki kuwa mstari wa mbele kuwasaidia wananchi kupata haki.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI, Yassin Ally amesema mbali na wananchi kushindwa kumudu gharama za kupata huduma za kisheria, pia wanakumbana na changamoto ya lugha ya kiingereza inayotumika kwenye migogoro ya kisheria.

Ally amewahimiza wananchi kupata ushauri wa kisheria kutoka kwa wasaidizi wa kisheria ambao wanapatikana hadi ngazi ya Kata kote nchini kabla ya kuingia kwenye migogoro mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalii (kulio) akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima (hayuko pichani) kwenye maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria na Siku ya Kujitolewa Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, Novemba 05, 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria na Siku ya Kujitolewa Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Mratibu Mkuu wa Mradi wa Kujitolea wa Umoja wa Mataifa (UN Volunteers Programme) nchini Tanzania, Christian Mwamanga akizungumza kwenye maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria na Siku ya Kujitolewa Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Shirika la VSO, Doris Kibasa akitoa salamu kwenye kwenye maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria na Siku ya Kujitolewa Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Mmoja wa wafanyakazi wa kujitolea kutoka shirika la Umoja wa Mataifa (UN) upande wa Zanzibar, Chizaro Bongobuliho akielezea umuhimu wa wafanyakazi wa kujitolea katika kuisaidia jamii.
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke akitoa salamu kwenye maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria na Siku ya Kujitolewa Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke (kulia) ni miongoni wa waliopokea tuzo za wafanyakazi wa kujitolea zilizotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kwa kushirikiana na Shirika la KIVULINI kupitia Mradi wa Kujitolea wa Umoja wa Mataifa (UN Volunteers Programme).
Mwandishi wa Habari jijini Mwanza, Sophia George akipokea tuzo kutoka kwa mgeni rasmi.
Mmoja wa wafanyakazi wa kujitolea kutoka shirika la KIVULINI akipokea tuzo ya kutambua mchango wa wafanyakazi wa kujitolea.
Wafanyakazi wa kujitolea kutoka mashirika mbalimbali wamepokea tuzo kutoka shirika la umoja wa Mataifa (UN) kwa kushirikiana na shirika la KIVULINI kupitia Mradi wa Kujitolea wa Umoja wa Mataifa (UN Volunteers Programme).

No comments:

Powered by Blogger.