LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jamii yatakiwa kutowafanyia ukatili wa lishe mama na mtoto

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com 
Imeelezwa kuwa ili mama aweze kubeba ujauzito salama na kujifungua salama suala la lishe ni muhimu na jambo linalotakiwa kupewa uzito wa hali ya juu na jamii inayomzunguka.

Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa shirika la Uzao Wetu Bwana Hassan Mtobela wakati akizungumzia siku 16 za kupinga ukatili ambapo amesema kuna wakati jamii inawafanyia ukatili wa lishe mama na mtoto.

Bwana Mtobela amesema kunakosa ambalo jamii imekuwa ikifanya wakati mama anapokuwa mjamzito kwa kuacha kumpatia mlo kamili ambao ni muhimu kwa kuwa husaidia mama kujifungua salama na kusaidia makuzi ya mtoto akiwa tumboni.

Amesema kile anachokula mama wakati akiwa mjamzito ndicho ambacho mtoto anakula pia hivyo chakula huamua mtoto aweje baada ya kuzaliwa.
“Mtoto anapokua na ubongo wake unakua na huwa hausubiri hivyo ni muhimu sana kwa jamii kuhakikisha mama anakula vyakula ambavyo vitaweza kusaidia kujenga ubongo wa mtoto akiwa tumboni na matokeo utayaona pia baada ya mtoto kuzaliwa” alisema Mtobela.

Kwa upande wake Bibi Getruda Ndalifashe ambae Muuguzi na Mkunga amesema ni muhimu kwa mama mjamzito kupewa mlo kamili ambao utasaidia ukuaji wa mtoto akiwa tumboni.

Bibi Ndalifashe amesema katika kipindi cha ujauzito mama anatakiwa kula vyakula vya kumuongezea nguvu pamoja na vyakula vya kumpatia joto yeye pamoja na mtoto.

Amesema mtoto anapokuwa tumboni anakula chakula kile ambacho mama anakula kupitia plasenta hivyo ni vema vyakula vyote atakavyokula mama viwe na manufaa kwake na upande wa mtoto.

“Mama anatakiwa atumie vyakula vinavyongeza nguvu pamoja Joto mfano Ndizi,Ugali,Viazi,Mafuta ya Samaki,Mafuta ya Karanga na vyakula vya Protin ikama vile Samaki,Dengu,Njegele na vyakula vya kumkuza mtoto ni kama Maziwa ,Mayai na vyakula vingine” alisema Bibi Ndalifashe.

Amesema katika kipindi cha ujauzito wazazi au jamii inayomzunguka mama mjamzito inaweza kuamua inataka mtoto wao aweje kulingana na chakula ambacho mama atakula na matokeo yataonekana baada ya mtoto kuzaliwa.

“Kitaalamu tunasema ubongo wa mtoto hukua kwa kasi katika siku 1000 za mwanzo za uhai wa binadamu,hapo unaweza kuona kumbe tunatakiwa kuwekeza mara tu mimba inapotungwa”.alisema Bibi Ndalifashe

Ripoti mpya ya ulimwengu iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto iitwayo Siku za Mwanzo za Miasha ya Kila Mtoto ni Muhimu.

Inasema kipindi cha tangu kutungwa mimba hadi kuanza shule ni muhimu na wakati wa ujauzito ni nafasi pekee katika kuandaa ubongo wa mtoto kwa kuwekeza kwenye lishe na afya kwa ujumla.
Na Alphonce Tonny, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.