LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwanza wahimizwa kuchukua hatua kukabiliana na maambukizi ya VVU

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Afisa Programu Shirika la KIVULINI, Grace Mussa (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima (kulia) kuhusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo Shirika hilo.
***

Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima amewahimiza wananchi kujiepusha na tabia hatarishi ikiwemo ngono zembe pamoja na kuwa na wapenzi wengi kwani zinachochea ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Malima ametoa rai hiyo Alhamisi Disemba 01, 2022 wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kwa Mkoa Mwanza katika uwanja wa Mirongo wilayani Nyamagana.

"Tutafakari mambo gani yanachangia kiwango cha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Mkoa wetu na tuchukue hatua ili kudhibiti ongezeko la maambukizo hayo kwani bado yako juu ya kiwango cha kitaifa" amesema Malima.

Malima ameeleza kiwango cha maambukizi ya VVM mkoani Mwanza ni asilimia 7.2 ikiwa ni ongezeko la juu ikilinganishwa na kiwango cha kitaifa ambacho ni asilimia 4.7 hivyo jitihada zaidi ikiwemo elimu zinahitajika ili kupunguza kiwango cha maambukizi.

"Elimu inatolewa kila mwaka, hatutachoka kuambizana kuhusu elimu ya kujikinga na maambukizi ya VVU, wananchi tunapopata elimu hiyo tukaifanyie kazi" amesema Malima huku akilipongeza Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU (NACOPHA) kwa jitihada za kuelimisha na kufuatilia makundi mbalimbali ya wanaoishi na VVU.

Akisoma risala kwenye maadhimisho hayo, Katibu wa WAVIU Konga ya Nyamagana Joseph Kiarata amesema jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika ikiwemo kuelimisha jamii njia sahihi za kujikinga na maambukizi ya VVU ingawa changamoto mila hasi ikiwemo kurithi wajane bado ni changamoto inayoeneza maambukizi hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji na ulawiti vina uhusiano wa karibu na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na hivyi kushauri Sheria kali kuchukuliwa kwa wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kwa Mkoa Mwanza katika uwanja wa Mirongo wilayani Nyamagana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika ka KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani 2022 jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika ka KIVULINI, Yassin Ally (kulia) akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani. Walioketi ni viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima (wa pili kushoto).
Katibu wa WAVIU Konga ya Nyamagana mkoani Mwanza, Joseph Kiarata akisoma risala wakati wa Maadhimisho ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kwa Mkoa Mwanza katika uwanja wa Mirongo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima (kushoto) kuhusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo katika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji ambavyo ni miongoni mwa njia zinazoeneza maambukizi ya VVU kwa wahanga wa vitendo hivyo.
Afisa Programu kutoka Shirika la WoteSawa (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima kuhusiana na shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
Jumbe mbalimbali katika banda la shirika la KIVULINI zikilenga kuhamasisha jamii kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima (kulia) akijionea shughuli mbalimbali za uzalishaji mali baada ya kutembelea banda la Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Maambukizi ya VVU (NACOPHA).

Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kwa Mkoa Mwanza katika uwanja wa Mirongo.

No comments:

Powered by Blogger.