LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanawake kampuni ya BOART LONGYEAR watoa msaada Gereza Kuu Butimba, Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wanawake wafanyakazi kutoka kampuni ya kimataifa ya BOART LONGYEAR inayojishughulisha na utoaji huduma ya uchimbaji madini (Drilling) katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, wametoa msaada wa mahitaji kwa ajili ya wafungwa katika Gereza Kuu la Butimba jijini Mwanza. 

Mmoja wa wanawake hao, Magreth Bugeraha ambaye ni Msaidizi wa Utawala wa kampuni hiyo alisema msaada huo ambao unajumuisha magodoro 50, taulo za kike katoni 10, sabuni za miche katoni tatu, sabuni za unga mifuko miwili na kandambili unalenga kuwakumbusha wafungwa kwamba jamii haijawatenga hivyo wasikate tamaa wakiwa gerezani.

Magreth aliongeza kuwa msaada huo pia ni sehemu ya wanawake hao kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo kilele chake ilikuwa Machi 08, 2023 na hivyo kutumia fursa hiyo kutoa rai kwa wafungwa kuendelea kuwa waadilifu huku wakitambua kwamba kuna maisha baada ya kumaliza vifungo vyao.

Naye Mkuu wa Gereza Kuu la Butimba, Deogratius Maguza alitoa shukurani za dhati kwa wanawake hao na kampuni ya Boart Longyear kwa kuguswa na kutoa msaada huo na kuomba wadau wengine kuiga mfano huo mwema.

Maguza pia alibainisha kuwa gereza hilo limekuwa likitoa mafunzo mbalimbali wafungwa ili kuwajengea uwezo wa kuanzisha shughuli mbalimbali za uzalishaji mali baada ya kumaliza vifungo vyao.

Kwa upande wao wafungwa wa Gereza Kuu Butimba waliwapokea kwa furaha wanawake wafanyakazi wa kampuni ya Boart Longyear na kuwashukuru kwa msaada waliowafikishia.

Katika makabidhiano hayo, wanawake wafanyakazi wa kampuni ya Boart Longyear walifurahishwa na kiwanda cha Gereza Kuu Butimba cha utengenezaji bidhaa mbalimbali ikiwemo viatu, batiki, mikeka pamoja na samani na kuahidi kuunga mkono jitihada hizo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wanawake wafanyakazi kutoka kampuni ya Boart Longyear wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Gereza Kuu la Butimba, Deogratius Maguza baada ya kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo magodoro, sabuni na taulo za kike (pads) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2023.
Wanawake wafanyakazi kutoka kampuni ya Boart Longyear wakishusha magodoro baada ya kuwasili katika Gereza Kuu la Butimba jijini Mwanza.
Wanawake wafanyakazi kutoka kampuni ya Boart Longyear wakishusha magodoro baada ya kuwasili katika Gereza Kuu la Butimba jijini Mwanza.
Wanawake wafanyakazi kutoka kampuni ya Boart Longyear wakiwa katika viunga vya Gereza Kuu Butimba kwa ajili ya kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wafungwa.
Wanawake wafanyakazi kutoka kampuni ya Boart Longyear wakiwa katika viunga vya Gereza Kuu Butimba kwa ajili ya kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wafungwa.
Baadhi ya wanawake wafanyakazi kutoka kampuni ya Boart Longyear wakiwa katika viunga vya Gereza Kuu Butimba kwa ajili ya kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wafungwa.
Baadhi ya wanawake wafanyakazi kutoka kampuni ya Boart Longyear wakiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa wa Gereza Kuu Butimba jijini Mwanza.
Baadhi ya wanawake wafanyakazi kutoka kampuni ya Boart Longyear wakiwa kwenye fukwe ya Stress Free inayomilikiwa na Gereza Kuu Butimba baada ya kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wafungwa wa gereza hilo.
Baadhi ya wanawake wafanyakazi kutoka kampuni ya Boart Longyear wakiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa wa Gereza Kuu Butimba jijini Mwanza wakiongozwa na Mkuu wa Gereza hilo, Deogratius Maguza (katikati mbele).

No comments:

Powered by Blogger.