LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkurugenzi Cecy Toto & Gift Shop awaunga mkono Wanahabari Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji bidhaa za watoto ya Cecy Toto & Gift Shop, Cecilia Melchior ameungana na waandishi wa habari wanawake mkoani Mwanza kwa kuchangia mahitaji mbalimbali ikiwemo vyakula kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika Kituo cha Nyumba ya Matumaini Nyegezi.

Itakumbukwa katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani 2023, waandishi wa habari wanawake mkoani Mwanza walikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali katika Kituo hicho cha kulelea watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Miongoni mwa mahitaji yaliyokabidhiwa ni pamoja na mchele kilo 100, sukari kilo 50, sabuni za mche boksi 10, mafuta ya kula Lita 40, juisi katoni 15 na mafuta ya kupaka mwili katoni mbili.

Cecy aliungana na waandishi hao kupitia uratibu wa chama (Mwanza Press Club- MPC) na kutumia fursa hiyo kutoa rai kwa wadau mbalimbali kuwasaidia watu wenye uhitaji kwani hiyo ndiyo sadaka ya kweli.

Cecy alisema ni vyema elimu ukaendelea kutolewa jamii hususani wanawake ili kutambua umuhimu wa kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito na kuzingatia matumizi ya vyakula jamii ya protini ili kuwakinga watoto kuzaliwa na tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi.
#BMGHabari
Mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji bidhaa za watoto ya Cecy Toto & Gift Shop iliyopo jijini Mwanza, Cecilia Melchior (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Kituo cha kulea watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi cha Nyumba ya Matumaini Nyegezi, Getruda Butondo (kushoto) na baadhi ya wazazi walio katika Kituo hicho.
Mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji bidhaa za watoto ya Cecy Toto & Gift Shop iliyopo jijini Mwanza, Cecilia Melchior akiwasili katika Kituo cha kulea watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi cha Nyumba ya Matumaini Nyegezi kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali ya vyakula.
Baadhi ya akina mama wakipokea sukari.
Mkurugenzi wa Cecy Toto & Gift Shop, Cecilia Melchior (mwenye nguo nyeusi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wazazi wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaokaa katika Kituo cha Nyumba ya Matumaini Nyegezi na Meneja wa Kituo hicho.

No comments:

Powered by Blogger.