LIVE STREAM ADS

Header Ads

TBS yawataka wazalishaji wa matofali, makaravati na wamiliki wa gereji kuzingatia ubora wa viwango

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com

Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya akifungua Mafunzo ya Uhamasishaji kwa Watengenezaji wa Matofali, Makaravati na Wamiliki wa Gereji za Magari kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yaliyofanyika leo Machi 9,2023 katika Ofisi za TBS Kanda ya Mashariki Jengo la PSSF Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Uhamasishaji kwa Watengenezaji wa Matofali, Makaravati na Wamiliki wa Gereji za Magari kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yaliyofanyika leo Machi 9,2023 katika Ofisi za TBS Kanda ya Mashariki Jengo la PSSF Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya akisisitiza jambo wakati akifungua Mafunzo ya Uhamasishaji kwa Watengenezaji wa Matofali, Makaravati na Wamiliki wa Gereji za Magari kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yaliyofanyika leo Machi 9,2023 katika Ofisi za TBS Kanda ya Mashariki Jengo la PSSF Jijini Dar es Salaam

Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki TBS, Bw.Francis Mapunda akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Uhamasishaji kwa Watengenezaji wa Matofali, Makaravati na Wamiliki wa Gereji za Magari kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yaliyofanyika leo Machi 9,2023 katika Ofisi za TBS Kanda ya Mashariki Jengo la PSSF Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya akipata picha ya pamoja na watumishi wa TBS Kanda ya Mashariki wakati ufunguzi wa Mafunzo ya Uhamasishaji kwa Watengenezaji wa Matofali, Makaravati na Wamiliki wa Gereji za Magari kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yaliyofanyika leo Machi 9,2023 katika Ofisi za TBS Kanda ya Mashariki Jengo la PSSF Jijini Dar es SalaamMkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya akipata picha ya pamoja na Watengenezaji wa Matofali, Makaravati na Wamiliki wa Gereji za Magari kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani wakati akifungua Mafunzo ya wadau hao yaliyofanyika leo Machi 9,2023 katika Ofisi za TBS Kanda ya Mashariki Jengo la PSSF Jijini Dar es Salaam

*********

NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka Watengenezaji wa Matofali,Makaravati na wamiliki wa gereji za Magari kwa Mkoa wa Dar es salaam na Pwani kutoa huduma zinazozingatia viwango vinavyotakiwa ili kumlinda mlaji pamoja na kukuza uchmi wa nchi.

Akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya uhamasishaji kwa watengenezaji na wamiliki hao, Mkurugenzi wa TBS,Dkt Athumani Ngenya amesema kuwa huduma wanazotoa zinagusa maisha ya kila mwananchi moja moja hivyo ni lazima ziwe na ubora unaokubalika ili mlaji aweze kupata thamani ya pesa zake pia kuwepo na ushindani ili kuweza kunyanyua uchumi wa nchi.

Amesema kuwa idadi ya wadau wanaotoa huduma za utengenezaji wa Matofali,Makaravati na wamiliki wa Gereji za magari wanaotambuliwa na TBS ni kwa kiwango kidogo hivyo kupitia mafunzo hayo yawe chachu kwa waliofika kuwahamasisha wengine kuthbitisha kama walivyofanya wengine.

"Azma ya serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa na kuuzwa hapa nchini zinafanywa kwa kuzingatia viwango ili kumlinda mlaji pamoja na kukuza uchumi kwa ujumla.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki TBS, Bw.Francis Mapuda amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhimiza jinsi ya kufanya uthibitishaji wa ubora katika bidhaa wanazozalisha ili kuweza kutoa huduma zinazokubalika.

No comments:

Powered by Blogger.